Maduka ya Taifa ya Dawa ( National Medical Stores) iliharibu dawa na vifaa vingine vyenye thamani ya zaidi ya dola milioni 86 mwaka 2023/24 / picha: NMS

Benki ya Dunia imekataa ombi la Uganda la kuelekeza fedha za ruzuku ya Uviko 19 katika kukamilisha miradi ya miundombinu ya afya iliyokwama, Waziri wa Afya Dkt. Ruth Aceng amefichua.

Dkt. Aceng alieleza kusikitishwa kwake na hatua hiyo, wakati wa kikao na Kamati ya Bunge ya Afya kuhusu Waraka wa Mfumo wa Bajeti wa Wizara ya Afya wa 2025/2026.

Akielezea kuhusu miradi iliyokwama, Dkt. Aceng alisema kuwa, hao awali, fedha za Mradi wa Kukabiliana na Uviko 19 na Maandalizi ya Dharura ya Uganda (UCREV), zilikuwa zimetengwa kama ruzuku kwa Uviko 19 lakini hazikuweza kutumika tena.

"Tulifikiri tunaweza kupanga upya fedha kushughulikia miradi iliyokwama, lakini Benki ya Dunia ilikataa pendekezo letu. Mradi huo utafungwa itakapofika mwezi Juni 2025, licha ya mazungumzo tuliyofanya,” alieleza Dkt. Aceng.

Haya yanajiri wakati ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Disemba 2024 ikifichua kuwa Bohari Kuu ya Madawa nchini Uganda, iliharibu chanjo za Uviko 19, dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARVs) na vifaa vya majaribio vilivyokwisha muda wake, vyenye thamani ya zaidi ya dola milioni 86, kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Hiili ni ongezeko la zaidi ya dola milioni 8 ya zile zilizoharibiwa mwaka uliopita.

Hali mbaya ya afya

Katika hatua nyingine, wabunge nchini Uganda wameonesha wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya vituo vya afya, ikitaja uchakavu, ukosefu wa vifaa muhimu vya matibabu, na mashine kutofanya kazi.

“Inasikitisha kwamba baadhi ya hospitali za rufaa za mikoa hazina vitengo maalumu vya dharura. Kitengo cha Soroti hakipo, na ukumbi wake ni mdogo sana, na kuwalazimu wagonjwa kupanga foleni kwa ajili ya upasuaji," alisema Isaac Otimgiw, mbunge wa eneo la Padyere.

Pia aliangazia ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti vya kisasa, akidokeza kuwa, inailazimy Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arua kuhifadhi miili katika Hospitali Kuu ya Nebbi.

"Sehemu za kimsingi kama mashine za X-ray huko Moroto zimepungua kwa zaidi ya miezi sita, huku tukikosa majibu ya uhakika kuhusu ni lini vifaa hivi vitapatikana," aliongeza.

Waziri wa afya Dkt. Aceng alitaja ufadhili mdogo kuwa kikwazo kikubwa.

“Tulipokea takriban dola laki 543 (UGX bilioni 2) pekee kununua vifaa nchi nzima. Baadhi ya mashine zimeacha kutumika kutokana na ukosefu wa fedha. Tunahitaji rasilimali za ziada ili kufunga mashine za X-ray na vifaa vingine muhimu,” alisema.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika