Bara la Afrika linajivunia kuwa na zaidi ya ng'ombe milioni 300, hivyo kuwa moja ya wazalishaji wakubwa zaidi wa nyama ulimwenguni.
Afrika inakadiriwa kuzalisha takriban tani milioni 7.5 za nyama ya ng'ombe kwa mwaka. Ethiopia ndio kinara kwa idadi ya ng’ombe barani Afrika na ya tano duniani. Benki ya Dunia inasema Ethiopia in zaidi ya ng’ombe milioni 70.3.
Inafuatiwa na Tanzania ambayo ina takrbain ng’ombe milioni 36.6. Hata hivyo, kuwa na idadi kubwa ya ng’ombe haina maana kuwa wanaongoza katika uzalishaji wa nyama kwa ajili ya mauzo.
![](https://images-cdn.trtworld.com/trtafricaswa/5399795_1403-0-3617-3262.jpeg)
Takwimu za 2023 zinaonyesha kuwa Afrika Kusini ndio inayoongoza katika uzalishaji wa nyama kwa zaidi ya tani milioni 2.7.
Imefuatwa na Sudan na Ethiopia.
Lakini kwa nini nchi zenye idadi kubwa ya mifugo sio zenye uzalishaji mkubwa wa nyama.
Mbali na mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zenye ng’ombe, nchi hizo pia zina changamoto nyengine.
Ethiopia inayoongoza kwa idadi ya ng’ombe barani inauza nyama yake katika nchi za Falme za Kiarabu- UAE, Saudi Arabia, Hong Kong, Vietnam, Qatar, and nchi nyengine za Asia.
Serikali ya Ethiopia inakiri kuwa imepata dola bilioni 1.1 pekee kutoka sekta ya mifugo katika kipindi cha miaka 14 iliyopita.
Nchi hiyo, inasema machinjio makubwa na ya kisasa 12 iwapo yataendeshwa kwa ufanisi, basi yana uwezo wa kuuza nje zaidi ya tani 200 000 za nyama kila mwaka.
![](https://images-cdn.trtworld.com/trtafricaswa/14040018_0-0-5500-3667.jpeg)
Hata hivyo, machinjio hayo yanasindika na kusafirisha asilimia 10 tu ya uwezo wake kwa mwaka.
Hata hivyo, machinjio hayo yanasindika na kusafirisha asilimia 10 tu ya uwezo wake kwa mwaka.
Lawama zimepelekwa kwa sekta nyengine, ikiwemo mfumo mbovu wa masoko na usambazaji pamoja na kukosekana kwa uratibu miongoni mwa machinjio.
Tanzania nayo soko lake kubwa la nyama ni Comoros, Jordan Kuwait , UAE , Oman , Vietman , Hong Kong , Qatar na Saudi Arabia. Mauzo ya nyama ya Tanzania yameongezeka kwa kiasi kikubwa, kutoka tani 1,774.3 mwaka 2022 hadi tani 14,701.2 mwaka 2023.
Lakini hiki bado ni kiwango cha chini cha uzalishaji kulingana na mahitaji ya soko.
Upatikanaji mdogo wa ardhi kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa malisho, ikiwa ni pamoja na maeneo ya malisho, maambukizi makubwa ya magonjwa ya mifugo, upatikanaji duni wa mikopo ya shamba, miundombinu duni, mfumo duni wa masoko, mashirika dhaifu ya wafugaji wa ng’ombe, huduma duni za kitaalamu na uwezo mdogo wa kimaumbile.
Ng'ombe wa kienyeji ndio fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa nyama ya ng'ombe.
Wataalamu wanashauri kuwa kuwekeza zaidi katika kulea mifugo na kuzalisha nyama kutaongeza uwezo wa nchi hizi kuzalisha nyama zaidi na hapo kupanda katika ngazi ya wauzaji wakuu wa nyama duniani.Friday, July 19th