Siku ya Jumapili, Afrika Kusini ilitwaa rasmi Afrika Kusini Jumapili ilitwaa rasmi Urais wa G20, huku Rais Cyril Ramaphosa akiielezea nafasi hiyo kama muhimu kwa taifa hilo.
Afrika Kusini inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuongoza kundi la mataifa yenye nguvu, maarufu kama G20.
" Licha ya uchumi wetu kuwa mdogo, sisi ni sehemu ya G20," alisema Rais Ramaphosa wakati akizungumza na wandishi wa habari katika eneo la Thabazimbi katika jimbo la kaskazini la Limpopo.
Alisema nchi za G20 zinachangia asilimia zipatazo 75 za biashara ulimwenguni jambo ambalo ni fursa nzuri kwa Afrika Kusini. Ramaphosa pia aliahidi kufanya kazi kwa ukaribu na Rais mteule wa Marekani Donald Trump, akigusia kuwa Marekani itakuwa Rais wa G20, ifikapo mwaka 2026.
Wiki mbili zilizopita, Ramaphosa alisema kuwa atatumia nafasi ya uongozi wa Afrika Kusini ndani ya G20 katika kukuza ukuaji wa uchumi jumuishi na maendeleo endelevu, na kwamba Pretoria imepitisha "mshikamano, usawa na uendelevu" kama dhima yake wakati ikishika hatamu ya G20.
Kulingana Ramaphosa, Afrika Kusini itaendelea kuimarisha na kuendeleza harakati za pamoja za Malengo ya Maendeleo Endelevu.
"Iwe ni Gaza, Sudan, au Ukraine, lazima sote tusimame katika mshikamano na watu hao ambao wanakabiliwa na shida na mateso," Ramaphosa alisema, akiongeza kuwa ni lazima kwa G20 kuunga mkono nchi zilizo hatarini .