Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa serikali ya Afrika inatambua jitihada za Palestina kutaka uhuru wao / Picha: Reuters

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa serikali ya Afrika inatambua jitihada za Palestina kutaka uhuru wao,

Mgogoro kati ya Israel na wapiganaji wa Hamas tangu tarehe 7 Oktoba, umezua mgogoro mpya kati ya Israel na Palestina huku nchi tofauti duniani zikitangaza misimamo yao,

"Tumesimama hapa kama uongozi wa chama cha African National Congress tukielezea wasiwasi wetu kuhusu kile kinachoendelea," Rais cyrila Ramaphosa ameelezea waandishi wa habari.

"Mvutano unatokea pande zote lakini tunaahidi msimamo wetu na Wapalestina kwa sababu wana mapambano ya haki na haki yao ya kibinadamu inakiukwa na vile vile harakati zao za kujitawala ni kitu ambacho tumekiunga mkono kila wakati," Ramaphosa ameongezea.

Afrika Kusini imetangaza msimamo wake wa kuunga Palestina mkono tangu 1994 wakati chama cha African National Congress, ANC kilipoingia madarakani.

Msimamo huu umeifanya nchi hiyo kuwa moja ya sauti maarufu zinazoikosoa Israel duniani kote.

"Suluhisho la pekee kati ya Israel na Palestine hasa ni uwepo wa mataifa mawili, kulingana na mipaka ya 1967 kama ilivyopitishwa na jamii ya kimataifa na Umoja wa mataifa," Rais Ramaphosa amesema.

Afrika Kusini imesema iko tayari kusaidia upatanishi kati ya Israel na Palestina.

TRT Afrika