Afrika Kusini imelaani mwendelezo wa mashambulizi kwenye hospitali na vituo vingine vya kutolea huduma za afya huko Palestina na kusema, na kusisitiza kuwa Tel Aviv inakwenda kinyume na maamuzi ya hivi karibuni yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
"Mashambulizi dhidi ya vituo vya hospitali yanakwenda kinyume kabisa na uamuzi wa ICJ. Ukiharibu hospitali, na kudai kuwa waliojeruhiwa hawapaswi kupata msaada wowote. Kwamba watu wanaohitaji matibabu lazima wasiwe nayo, kwa hivyo, kimsingi unawahukumu watu kifo kutokana na shughuli zako," Waziri wa Mambo ya Nje Naledi Pandor alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria.
Vikosi maalum vya Israel vilivamia hospitali moja katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuua watu watatu, mapema wiki hii.
Afrika Kusini yaikana Iran
"Na jambo la kushangaza kuona umevaa kama mhudumu wa afya na kwenda kuungamiza watu," alisema Pandor.
Wiki iliyopita, ICJ iliiamuru Israel kuchukua "hatua zote ndani ya uwezo wake" kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki huko Gaza lakini ikakosa kuamuru kusitishwa kwa mapigano.
Pandor alikanusha ripoti kwamba Iran ilifadhili timu ya wanasheria ya Afrika Kusini iliyofungua shauri dhidi ya Israel katika Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa.
"Ninachojua, timu ya wanasheria bado haijalipwa, na sijaona wito kutoka Iran kwa malipo hayo," alisema kwa kejeli.
Pandor alisema wapinzani wa Afrika Kusini wamemtukana na kumuita kila aina ya maneno kwa msimamo wa serikali yake.
Alisema baadhi wamekuwa wakimuita mwanachama wa kundi la kigaidi la ISIS/Daesh na mfuasi wa Hamas, na kwamba lazima Israel iwajibike kama haitozingatia maagizo kutoka ICJ.