Mahakama ya Afrika Kusini imeiamuru serikali kuhakikisha kwamba usambazaji wa umeme katika hospitali za umma, shule na vituo vya polisi unabaki bila kukatizwa.
Uchumi mkubwa zaidi wa viwanda barani Afrika umekuwa ukishuhudia uhaba wa umeme ambao haujawahi kushuhudiwa huku kukiwa na madai ya ufisadi katika kampuni kubwa ya nishati inayomilikiwa na serikali, Eskom. Kukatika kwa umeme kunaweza kudumu hadi saa 15 kwa siku.
Majaji wa mahakama kuu mnamo Ijumaa walimwagiza waziri wa mashirika ya umma "kuchukua hatua zote zinazofaa" ndani ya siku 60 kutii agizo hilo.
Walisema "kumekuwa na ukiukwaji unaorudiwa na hali ya majukumu yake ya kikatiba na kisheria na kwamba ukiukaji huu unaendelea kukiuka haki za raia za afya, usalama na elimu".
Ilifuata kesi ya vyama vya upinzani, NGOs na watu binafsi dhidi ya serikali.
Rais Cyril Ramaphosa mwezi Machi alimteua waziri wa kwanza wa umeme nchini humo katika jitihada za kutatua tatizo la umeme. Chama tawala cha ANC kinakabiliwa na shinikizo la kukabiliana na mzozo huo kabla ya uchaguzi mwaka ujao.