Barbra Banda wa Zambia (kushoto) na Ademola Lookman wa Nigeria walishinda tuzo za Wachezaji Bora wa CAF. /Picha: CAF

Na Charles Mgbolu Msisimko wa kusisimua ambao matukio ya michezo huleta barani Afrika haukupungua mwaka wa 2024, huku rekodi za zamani zikivunjwa na vipaji vipya vya nyumbani vkatika vitabu vya rekodi za historia ya michezo.

Mwaka unapomalizika, TRT Afrika inakuletea baadhi ya matukio muhimu ya kimichezo ambayo yamefanya mwaka wa 2024 kuwa wa ajabu.

Wababe wa AFCON

Mwaka ulianza kwa kampeni ya kusisimua ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ambayo ilianza Januari.

Wanasoka wa Timu ya Taifa ya  Ivory Coast walishinda kombe la AFCON 2024 licha ya kuanza michuano hiyo vibaya. /Picha: Getty

Mashindano hayo, ambayo yalifanyika nchini Ivory Coast, baada ya miongo minne, yalishuhudia wenyeji wakinyakua taji la tatu la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mechi ya fainali 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara jijini Abidjan.

Ilikuwa ni ushindi uliotokana na hali ngumu wakati Wana Ivory Coast walipoondolewa katika kundi lao kufuatia kushindwa mara mbili, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa mabao 4-0 na Equatorial Guinea.

Washindi wa kanda

Ukanda wa Afrika Kaskazini, kwa upande wao, ulipata ushindi mkubwa, huku klabu ya Zamalek ya Misri ikitwaa ubingwa wa CAF Super Cup wa 2024 kufuatia ushindi mnono wa mikwaju ya penalti dhidi ya wapinzani wao Al Ahly baada ya muda wa kawaida wa mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Vigogo wa Misri, Al Ahly pia walishinda taji la 12 la Ligi ya Mabingwa Afrika lililoongeza rekodi baada ya kuifunga Esperance 1-0 katika mechi ya mkondo wa pili wa fainali mjini Cairo.

Olimpiki na Paralimpiki

Bara hilo pia lilifanya vyema katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, huku Afrika ikiibuka na jumla ya medali 35, zikiwemo13 za dhahabu, 12 za fedha na 14 za shaba.

Tuzo ya mwanariadha aliyejitahidi zaidi katika Olimpiki inaweza kupewa Letsile Tebogo wa Botswana, ambaye alishinda medali ya kwanza ya dhahabu barani Afrika katika mbio za mita 200 na pia kupata rekodi ya Kiafrika.

Letsile Tebogo wa Botswana alivunja rekodi ya dunia ya mita 200. /Picha: Letsile (Instagram)

Mwanariadha wa Kenya Emmanuel Wanyonyi pia alipata mafanikio mengine ya ajabu kwani alikuwa mwanariadha mwenye umri mdogo zaidi kushinda Olimpiki, akitwaa taji hilo akiwa na umri wa miaka 20, akimshinda Marco Arop wa Kanada, bingwa wa zamani wa dunia.

Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Paris 2024 pia ilikuwa muhimu kwa Afrika, kwani bara lilifanikiwa kupata jumla ya medali 64, moja zaidi ya michezo ya awali ya Tokyo 2020.

Tuzo na kutambuliwa

Shangwe zilidhihiri kwenye Tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) 2024. Mshambulizi wa Nigeria Ademola Lookman alitangazwa kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka baada ya kufanya vizuri kwa klabu yake na timu ya taifa.

Barbra Banda wa Zambia pia alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kike wa Afrika wa Mwaka.

Ronwen Williams wa Afrika Kusini alikuwa mshindi wa pekee mara mbili katika Tuzo za CAF 2024. Picha: Rowen (Instagram)

Hafla hiyo pia ilishuhudia wanasoka wengine wa Kiafrika wenye vipaji, kama vile kipa wa Afrika Kusini Ronwen Williams, kuwa mshindi mara mbili pekee usiku huo, akitwaa Tuzo za Kipa Bora wa Mwaka wa Wanaume na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu ya Wanaume.

Chiamaka Nnadozie wa Nigeria alishinda tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka wa Wanawake kwa mwaka wa pili mfululizo, baada ya kuwa na msimu mwingine bora kwa timu ya Paris FC ya Ufaransa, ambapo alitawazwa kuwa Kipa Bora wa Ligi ya Première kwa Msimu wa 2023-24.

Nigeria pia ilishuhudia gumzo la vyombo vya habari kuhusu uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji Victor Osimhen kutoka Napoli kwenda kwa miamba wa klabu ya Galatasaray ya Uturuki.

Vifo

Cha kusikitisha ni kwamba mwaka wa 2024 pia ulirekodi misiba yenye kuhuzunisha.

Mwanariadha wa Kenya Kipyegon Bett, ambaye alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 800 kwenye Mashindano ya Dunia ya 2017 jijini London, aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 26 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Rebecca Cheptegei alikufa siku tatu baada ya kushambuliwa. /Picha: Wengine

Mwanariadha wa Uganda wa mbio za Olimpiki Rebecca Cheptegei pia alifariki baada ya kushambuliwa kwa moto na mpenzi wake nje ya nyumba yake huko Eldoret, Kenya.

Vurugu za mashabiki

2024 pia ilishuhudia matukio kadhaa ya vurugu ya mashabiki ambayo yalisababisha vifo. Takriban watu wanane waliuawa katika mkanyagano mwezi Julai katika uwanja wa mpira wa miguu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, wakati wa mechi kati ya timu mbili za Senegal.

Mapambano yalizuka kati ya mashabiki wa wapinzani wa US Ouakam na Stade de Mbour kwenye uwanja wa Demba Diop, na polisi walifyatua mabomu ya machozi kujaribu kutuliza mapambano hayo.

Tukio kama hilo la mkanyagano pia lilisababisha vifo vya takriban watu 56 na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa ghasia na mkanyagano katika uwanja wa soka kusini mashariki mwa Guinea, serikali ilisema mwezi Disemba.

Mashindano ya Formula One

Aidha mwaka wa 2024 umemalizika kwa habari nzuri sana, Rais Paul Kagame wa Rwanda alitangaza mnamo Desemba nchi yake itajitolea kuwa mwenyeji wa mashindani ya magari ya Formula One katika mji mkuu, Kigali, mnamo 2025.

Taifa hilo likifuatilia kwa dhati mipango ya kuandaa mashindano ya F1 Grand Prix, yanayolenga kurudisha mchezo huo barani Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1993.

TRT Afrika