Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan anatarajiwa kutembelea Ethiopia tarehe 3, Agosti 2024, na kuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Taye Atske Selassie, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema.
Waziri wa Mambo ya Nje Fidan, anatarajia kuwa na mazungumzo ya nchi mbili, maridhiano na Somalia na mambo mengine ya kikanda, wakati za ziara yake nchini Ethiopia.
Mwezi uliopita, Hakan Fidan alikuwa mwenyeji kwa wenzake wa Ethiopia na Somalia mjini Ankara ambapo watatu hao walitia saini taarifa ya pamoja kufuatia mazungumzo ya "wazi, wema na ya mbele" kuhusu tofauti zao.
Wakati wa mkutano wa Julai, mawaziri wa Somalia na Ethiopia walijadili njia za kushughulikia tofauti zao "ndani ya mfumo unaokubalika" na kukubaliana kufanya duru nyingine ya mazungumzo huko Ankara, Septemba 2.
Mahusiano ya Kidiplomasia ya Uturuki
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Ethiopia, ambao una umuhimu mkubwa katika Sera ya Ushirikiano ya Afrika ya Uturuki, ulianzia nyakati za kabla ya Jamhuri, haswa 1896.
Ubalozi wa Uturuku mjini Addis Ababa ulianzishwa mwaka 1926, wakati ule wa Ethiopia mjini Ankara ulifunguliwa mwaka1933. Ingawa ubalozi wa Ethiopia mjini Ankara ulifunga mwaka 1984 kulingana na mabadiliko ya uongozi, ulifunguliwa tena mwaka 2006.
Uhusiano kati ya Uturuki na Ethiopia umeimarika kupitia ziara mbalimbali za kirafiki.
Kiasi cha biashara
Ujazo wa biashara kati ya nchi hizo mbili, ambao ulifikia dola milioni 27 mwaka 2000, ulifikia kiasi cha dola milioni 345 mwaka 2023.
Kuna lengo kubwa la kuongeza idadi hii hadi dola bilioni 1 ndani ya miaka mitano ijayo. Uturuki ni miongoni mwa nchi nne za juu katika suala la Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) nchini Ethiopia, na maslahi yanayoongezeka kutoka kampuni za Uturuki.
Mvutano kati ya Ethiopia na Somalia
Ethiopia, nchi yenye watu wengi zaidi isiyo na bahari duniani, ilipoteza ufikiaji wake wa baharini baada ya kujitoa kwa Eritrea mnamo 1991 na uhuru wa mwaka1993.
Ufikijiaji wa Bahari Nyekundu bado ni suala muhimu la kiuchumi kwa Ethiopia.
Mnamo Januari 1, 2024, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais wa Somaliland walitia saini Mkataba wa Maelewano.
Wakati wa hafla ya kutia saini, Rais wa Somaliland alitangaza kuwa Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuitambua Somaliland, kauli ambayo ilileta upinzani mkubwa kutoka kwa Somalia na jumuiya ya kimataifa.
Msaada wa Uturuki kumaliza mgogoro huo
Mnamo Mei 8, 2024, Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Mulatu Teshome Wirtu, akiandamana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, alipokelewa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Wakati wa mkutano huo, Ethiopia iliomba uungwaji mkono wa Uturuki kuhusu mzozo wake na Somalia.
Kama mpatanishi anayeaminika, Uturuki, chini ya maagizo ya Rais Erdogan, alianzisha juhudi za upatanishi. Waziri wa Mambo ya Nje Fidan alifanya mazungumzo na mawaziri wenzao wa Ethiopia na Somalia, akiwakaribisha mawaziri wao wa mambo ya nje mjini Ankara mnamo Julai 1, 2024.
Hii ilikuwa mara ya kwanza baada ya miezi miwili ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yote mawili walionekana pamoja kwenye picha, na walitoa taarifa ya pamoja wakielezea nia yao ya kutatua mizozo yao kwa amani. Pia walionesha nia ya kukutana tena Ankara Septemba 2.
Jumuiya ya kimataifa imepongeza juhudi za Uturuki kuanzisha njia endelevu ya mazungumzo kati ya pande zote huku kukiwa na mvutano wa kikanda unaoongezeka.