Katika kikao chao siku ya Ijumaa, pembezoni mwa Mkutano wa 61 wa Usalama huko Munich, Fidan aliainisha msimamo wa Uturuki katika kupambana na ugaidi wa Daesh./Picha: AA  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, na kujadiliana naye hali ya Syria na Gaza, vyanzo vya kidiplomasia vimesema.

Katika kikao chao siku ya Ijumaa, pembezoni mwa Mkutano wa 61 wa Usalama huko Munich, Fidan aliainisha msimamo wa Uturuki katika kupambana na ugaidi wa Daesh.

Pia alisisitiza haja ya usitishwaji wa kudumu wa vita vya Gaza, akisema kuwa utatuzi wa mgogoro kati ya Israeli na Palestina ni wa muhimu kwa ajili ya amani ya kanda.

Suala la suluhu kati ya Urusi na Ukraine, pia lilijadiliwa wakati wa kikao hicho.

Mazungumzo ya Munich

Wakati huo huo, Fidan alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy na wa Ujerumani Annalena Baerbock, pembezoni mwa mkutano huo.

Katika kikao chake na Lammy, Fidan aliangazia umuhimu wa umoja wa Syria na umuhimu wa kuisaidia Syria baada ya kuangushwa kwa utawala wa Assad mwezi Disemba 2024.

Akizungumza na Baerbock, Fidan aligusia vita vya Ukraine na hali ya usalama nchini Syria.

TRT Afrika