Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki yatangaza uzinduzi wa kitabu kiitwacho "Diplomasia ya Amani ya Recep Tayyip”: Kisa mkasa cha Syria, kinachoangazia juhudi za Uturuki katika mgogoro wa miaka 13 wa Syria.
Kitabu hicho, kilichoandikwa lugha ya Kituruki, Kiarabu na Kiingereza, kinaangazi nafasi ya Uturuki katika kusukuma suala la haki na amani nchini Syria, chini ya uongozi wa Erdogan.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun alitangaz uzinduzi huo siku ya Alhamisi, akisisitiza msimamo wa Uturuki kuhusu umoja wa kisiasa na haki ya kujitawala ya watu wa Syria.
Alisisitiza kuwa mara zote, Uturuki imesimamia haki na ukweli katika janga la Syria.
Toka kuanza kwa mgogoro huo, Uturuki imechukua msimamo wa kibanadamu, ikitoa hifadhi kwa mamilioni ya wakimbizi wa Syria, huku ikipambana na magaidi.
Nafasi ya Uturuki kikanda na kimataifa
Chapisho hilo linaangazia mikakati ya Uturuki katika diplomasia ya kanda, ikiwemo majadiliano, misaada ya kibinadamu, na msimamo wake dhidi ya kuingiliwa na mataifa ya nje.
Pia, kinaangazia mikakati ya Uturuki katika usuluhishi na sera yake ya mambo ya nje kwa mustakabali wa Syria.
Kupitia kitabu hicho, Kurugenzi hiyo ya Mawasiliano inaangazia mchango wa Uturuki katika amani ya kanda na ulimwenguni .