Vikosi vya Usalama vya Uturuki vimewakata makali magaidi watano, akiwemo mmoja aliyekuwa anasakwa sana, katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
"Magaidi watano wamekatwa makali katika maeneo ya wilaya ya Dogubayazit katika jimbo la Agri na kijiji cha Palamut katika wilaya ya Hasankeyf kwenye jimbo la Batman, katika operesheni za 'BOZDOGAN-43' ," alisema Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya, kwenye ukurasa wa X siku ya Alhamisi.
Kati ya magaidi hao, yupo Yilmaz Oner, anayejulikana pia kwa jina la Sehmus Malazgirt, aliyewekwa kwenye kundi jekundu la wanaosakwa zaidi na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Kulingana na Yerlikaya, Oner alihusika katika jumla ya matukio 18 ya kigaidi yalioua maofisa usalama 27 na raia wanne, huku maofisa usalama 68 na raia wawili wakijeruhiwa.
Idara ya Kiintelejinsia ilisema kuwa Oner alitoa amri ya kutekelezwa kwa matukio hayo, aliongeza.
Magaidi wengine watatu waliokatwa makali katika operesheni hiyo walikuwa kwenye makundi ya rangi ya machungwa katika orodha ya Wizara, huku nyekundu ikiashiria wanaosakwa zaidi, ikifuatiwa na bluu, kijani, chungwa na kijivu.
Katika miaka 40 ya utekelezaji wake wa matukio ya kigaidi dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK kiliorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, huku likiwa limehusika na mauaji ya watu zaidi ya 40,000, wakiwemo wanawake na watoto wadogo.