Mamlaka za Uturuki hutumia neno “kukata makali” kuonesha kuwa magaidi walisalimu amri, kuuwawa au kukamatwa./ Picha: AA  

Vikosi vya ulinzi vya Uturuki vimewakata makali magaidi 32 kutoka kundi la PKK, kaskazini mwa Iraq, Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imesema.

Magaidi hao walilengwa katika maeneo ya Haftanin, Gara, na Hakurk, Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema kupitia ukurasa wake wa X, siku ya Ijumaa.

Imeongeza kuwa operesheni ya kukabiliana na ugaidi itaendelea "mpaka kila gaidi anaondolewa katika eneo hilo, bila kuruhusu mashirika ya kigaidi kupata nguvu tena."

Kikundi cha kigaidi cha PKK kinajulikana kwa kutumia eneo la kaskazini la Iraq, karibu na mpaka wa Uturuki kama sehemu yao ya kujificha.

Mamlaka za Uturuki hutumia neno “kukata makali” kuonesha kuwa magaidi walisalimu amri, kuuwawa au kukamatwa.

Katika kampeni yake ya takriban miaka 40 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK - kimeorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na Umoja wa Ulaya, kikiwa kimehusika na mauaji ya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake na watoto wachanga.

TRT Afrika