Msimamo wa Senegal kwa Palestina kuhusu uwepo wa dola kama suluhu ni wa "kuthaminiwa sana", Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.
“Tunafuatilia misimamo kutoka kwa ndugu zetu wa Afrika, ambao wanaoelewa kuhusu manyanyaso, vita na mauaji ya halaiki yanayatokana na sera za kimbari za Israeli,” alisema Erdogan siku ya Alhamisi kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenzake Bassirou Diomaye Faye wa Senegal.
Msimamo wa Senegal kwenye suala la Palestina ni wa kuthaminiwa sana, aliongeza Erdogan.
“Mabeberu wamejifunza kutoka Afrika kuwa amani haiwezi kujengwa kwa damu na mauaji ya halaiki,” alisema Erdogan akiongeza: “Ukweli huo huo pia utajidhihirisha Gaza na Lebanon.”
Kuhusu mashambulizi ya Israeli dhidi ya Lebanon na Palestina, Rais wa Uturuki alisema kuwa ukanda huo "unaelekea kwenye mchafuko makubwa," akionya kuwa hali itazidi kuwa mbaya sana siku zijazo.
Erdogan pia alizitaka nchi zote zenye "dhamira iliyo safi" kuongeza shinikizo dhidi ya serikali ya Israeli.