Uturuki yaokoa wahamiaji 27 wasio halali waliokataliwa na Ugiriki

Uturuki yaokoa wahamiaji 27 wasio halali waliokataliwa na Ugiriki

Wahamiaji waliokolewa katika pwani ya kaskazini magharibi mwa jimbo la Canakkale
Migrants in Greece / Photo: AA

Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Uturuki Jumapili kiliwaokoa wahamiaji 27 ambao walirudishwa kinyume cha sheria katika eneo la maji ya Uturuki na mamlaka ya Ugiriki.

Wahamiaji hao wa Afghanistan waliokolewa kutoka kwa boti karibu na wilaya ya Ayvacik kaskazini magharibi mwa mkoa wa Canakkale, kulingana walinzi wa Pwani.

Wahamiaji hao walipelekwa kwa mamlaka ya uhamiaji ya mkoa.

Uturuki na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamelaani mara kwa mara tabia haramu ya Ugiriki ya kuwarudisha wahamiaji wasiofuata utaratibu, ikisema inakiuka maadili ya kibinadamu na sheria za kimataifa kwa kuhatarisha maisha ya wahamiaji walio hatarini, wakiwemo wanawake na watoto.

Uturuki imekuwa eneo muhimu kwa wahamiaji wasio halali wanaotaka kuvuka kuingia Ulaya kuanza maisha mapya, hasa wale wanaokimbia vita na mateso.

AA