Mfululizo wa mashambulizi hayo na kukamatwa makali kwa magaidi ni dhihirisho la utayari wa Uturuki kuvunja himaya za za vikundi vya kigaidi vya PKK/KCK./Picha: AA  

Shirika la Kijasusi la Uturuki (MIT) limefanikiwa kuwakata makali gaidi mwandamizi wa PKK/KCK terrorist, Serkan Nazlier, katika operesheni iliyofanyika kaskazini mwa Iraq, vyanzo vya kiusalama vimesema siku ya Alhamisi. Nazlier, alikuwa ni ni mmoja wa watu wanaosakwa sana, huku akiongoza operesheni za PP, kusinimashariki mwa jimbo la Hakkari lilopo nchini Uturuki.

Mhusika mkuu wa mashambulizi hayo

Nazlier, ambaye alikuwa anajulikana kwa jina msimbo la "Sefkan Amed," alikuwa akiishi katika jimbo la Hakurk baada ya operesheni mfululizo za Kituruki ambazo ziliwatimua magaidi hao.

Mtu huyu ndiye alikuwa kinara wa kuratibu mashambulizi mbalimbali dhidi ya Uturuki, likiwemo shambulizi la kombora la mwaka 2019 kwenye ngome ya Jeshi la Uturuki iliyoko kaskazini mwa Iraq.

Moja ya kazi zake ilikuwa ni kuendesha operesheni mbalimbali, na kumfanya aendelee kutafutwa na majeshi ya Uturuki.

Mashambulio ya anga

Ukatwaji makali wa Nazlier ni sehemu ya mpango endelevu wa kukabiliana na ugaidi katika kanda hiyo.

Majeshi ya Uturuki yameimarisha operesheni, dhidi ya ugaidi, ikiwemo kurusha makombora ya angani dhidi magaidi 47 kaskazini mwa Iraq na Syria.

Toka Jumatano, jumla ya magaidi 59 kutoka vikundi cya PKK na PKK/YPG, wakiwemo viongozi wawili, ambao walikatwa makali, kulingana na Wizara ya Ulinzi.

Neno "kukatwa makali" hutumika na mamlaka za Uturuki kuashiria kuwa magaidi waliuwawa, kukamatwa au kusalimu amri.

Majibu ya shambulio la kigaidi mjini Ankara

Muendelezo wa mashambulizi ya naga yanafuatia tukio la kigaidi la Jumatano kwenye kiwanda cha anga cha Uturuki (TAI) mjini Ankara katika wilaya ya Kahramankazan.

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu watano na majeruhi 22, huku vyombo vya ulinzi vikijibu mapigo, kwa kuwakata makali magaidi wawili katika eneo la tukio.

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya, magaidi hao wametambulika kwa majina ya Mine Sevjin Alcicek na Ali Orek, ambaye anajulikana kwa jina msimbo Rojger, wote wakiwa ni wafuasi wa kikundi cha kigaidi cha PKK.

TRT Afrika