Uturuki yalaani mpango wa Israeli wa upanuzi wa milima ya Golan

Uturuki yalaani mpango wa Israeli wa upanuzi wa milima ya Golan

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imelaumu uamuzi wa Israeli wa kupanua eneo la Golan.
“Mpango wa Israeli unalenga kutia dosari jitihada za kuleta amani na utulivu nchini Syria," imesema wizara ya mambo ya nje. / Picha: AA  

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imelaani vikali uamuzi wa Israeli wa upanuzi wa makazi katika eneo la Golan, ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa Israeli toka mwaka 1967.

Katika taarifa yake, Wizara hiyo imeonesha wasiwasi mkubwa kutokana na mpango huo.

Hatua hiyo inaonesha vitendo vya Israeli katika ukanda huo, ikiwemo ukiukwaji mkubwa wa mkataba wa mwaka 1974.

“Vitendo hivyi vinaendelea kufifisha jitihada za kuleta amani nchini Syria na kuzidisha uhasama katika ukanda huo,” imesema wizara hiyo.

Taarifa hiyo imeziasa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua stahiki za kushugulikia ukiukwaji huo unaofanywa na serikali ya Netanyahu.

Kauli ya Uturuki inadhihirisha ongezeko la sintofahamu ya sera za Israeli katika eneo la Golan, eneo la kimkakati ambalo limehusika machafuko kwa muda mrefu.

TRT Afrika