Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imelaani "mauaji ya kinyama" ya kiongozi mwandamizi wa Hamas Ismail Haniyeh.
"Tunatuma sakamu zetu za rambirambi kwa watu wa Palestina waliojitoa sadaka kwa mamia ya mashahidi kama Haniyeh ili kuishi kwa amani, " ilisema wizara hiyo siku ya Jumatano.
Mauaji ya Haniyeh, kwa mara nyingine tena, yanadhihirisha serikali ya Israeli inayoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hana nia ya kutafuta amani, ilisema wizara hiyo.
Wizara hiyo, pia ilionya kuwa kanda hiyo itakabiliwa na migogoro mikubwa iwapo jumuiya ya kimataifa itashindwa kuithibiti Israeli.
"Uturuki itaendelea kuunga mkono jitihada za watu wa Palestina," iliongeza taarifa hiyo.
Mauji ya Haniyeh yanalenga kuongeza wigo wa migogoro, kwenda zaidi ya Gaza, ilisema.
Siku ya Jumatano, kikundi cha Hamas cha Palestina kilitangaza mauaji ya Ismail Haniyeh, kufuatia shambulio la anga lililonga makazi yake mjini Tehran, nchini Iran.
Kituo cha televisheni cha Iran, kilitanga taarifa za mauaji hayo, kikiongeza kuwa uchunguzi wake bado unaendelea na matokeo yake yatawekwa hadharani siku chache zijazo.