Uturuki inafuatilia kwa masikitiko kuhusu ajali ya helikopta iliyomhusisha Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
"Tunafuatilia kwa karibu tukio hilo huku tukiendelea kuwasiliana na mamlaka za Iran, na tuko tayari kutoa msaada wa muhimu," aliandika Erdogan kwenye ukurasa wa X kufuatia tukio hilo la Jumapili.
"Kwa niaba ya taifa langu, natoa salamu za pole kwa ndugu zetu na jirani zetu, watu wa Iran na serikali kwa ujumla, huku tukiwa na matumaini ya taarifa njema kutoka kwa Rais wa ujumbe wake haraka iwezekanavyo," aliongeza.
Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Nje alisema kuwa "misaada yote ya muhimu kwa ajili ya shughuli ya utafutaji na uokoaji ilikuwa imeandaliwa," kukiwa na matumaini kuwa Rais na ujumbe wa maofisa wa Iran, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian, wako salama salimini.
Moja kati ya helikopta tatu yaanguka
Mapema siku ya Jumapili, helikopta iliyokuwa imembeba Rasi wa Iran Ebrahim Raisi ilipata tatizo la kutua kutokana na hali mbaya ya hewa wakati inarudi kutoka shughuli ya kuzindua bwawa la mahi kwenye mpaka na Azerbaijan.
Hapo awali, kikosi cha Red Crescent cha Iran kilitangaza kuwa "ajali hiyo" ilitokea kati ya mpaka wa Kaleybar na Varzaqan. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi alisisitiza kuwa vikosi vya uokoaji vilikuwa havijafika katika eneo hilo.
Naibu Gavana wa Azerbaijan Mashariki Jabbarali Zakiri alisema kuwa helikopta mbili kati tatu zilizokuwa kwenye msafara wa Raisi zilifanikiwa kutua, wakati moja ikianguka.
Iliropotiwa kuwa, helikopta iliyokuwa imembeba Raisi ilikuwa na maofisa kadhaa, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian.