| Swahili
UTURUKI
2 DK KUSOMA
Uturuki yaelezea kusikitishwa na uvamizi wa Chuo Kikuu huko Prague
Takriban watu 15 waliuawa na wengine 24 kujeruhiwa katika shambulio la risasi lililofanyika Chuo kikuu Cha Charles mjini Prague.
Uturuki yaelezea kusikitishwa na uvamizi wa Chuo Kikuu huko Prague
Shambulio katika Chuo Kikuu Charles huko Prague / Picha: Reuters / Reuters
23 Desemba 2023

Uturuki imeelezea masikitiko yake kwa uvamizi wa risasi katika Chuo Kikuu kilichoko mji Mkuu wa Czech wa Prague na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10.

"Tunatoa rambirambi zetu kwa familia za waathiriwa na watu wa Czechia, na tunawatakia afueni ya haraka kwa wale waliojeruhiwa," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Oncu Keceli kupitia mtandao wa X.

Kauli yake imekuja baada ya watu wasiopungua 15 kuuawa na wengine 24 kujeruhiwa katika shambulio la risasi lililojiri katika Chuo Kikuu cha Charles katikati mwa Prague.

Mkuu wa Polisi Martin Vondrasek alisema kuwa mtu huyo mwenye silaha alikuwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24 katika Kitivo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Charles.

Mshambuliaji huyo alikuwa akiishi katika kijiji kilichokuwa kilomita 21 nje ya Prague, na baba yake alipatikana amekufa mapema leo.

CHANZO:TRT World