Vikosi vya usalama vya uturuki "vimewakata makali" magaidi 16 kaskazini mwa Iraq, Wizara ya Ulinzi ya taifa imesema, baada ya wanajeshi 12 wa Uturuki kuuawa kufuatia siku mbili za mashambulizi ya kigaidi.
Magaidi hao "walikatwa makali" ikimaanisha kuwa magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au walitekwa kupitia operesheni ya ukanda wa Claw-Lock, taarifa ya Wizara mnamo Jumamosi ilisema.
Uhusiano wa magaidi haukuelezwa, lakini kundi la kigaidi la PKK limejulikana kuwa linafanya harakati katika eneo hilo. Mara nyingi, magaidi wa PKK hujificha katika mpaka wa Kaskazini mwa Iraq ili kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Uturuki.
Katika taarifa ya baadaye, Wizara ilisema operesheni ya anga ilifanywa majira ya saa nne usiku dhidi ya malengo ya kigaidi kaskazini mwa Iraq na Syria, huku jumla ya malengo 29 ikiwa ni pamoja na mapango, makazi na maghala yaliyotumiwa na magaidi yaliharibiwa.
Maeneo yaliyolengwa yaligunduliwa kuwa yalikuwa na magaidi waliohusika na mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanachama wa juu, na magaidi wengi walikatwa makali, iliongeza.
Wizara hiyo ilisisitiza kuwa operesheni hiyo ilifanywa kwa mujibu wa haki ya Uturuki ya kujitetea inayotokana na kifungu cha 51 cha Umoja wa Mataifa na kila tahadhari ilichukuliwa kuhakikisha kuwa raia wasio na hatia, vitu vya kirafiki, mali ya kihistoria na kitamaduni na mazingira haviko hatarini.
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler aliongoza na kusimamia shughuli za anga kutoka kituo cha shughuli za Jeshi la anga ambacho kiliharibu makazi ya magaidi hao.
Guler aliwapongeza marubani ambao walifanikiwa kushambulia malengo, pamoja na makamanda wakuu wa vikosi vya jeshi la Uturuki.
Zaidi ya watu 40,000 wauawa Katika kampeni ya kigaidi ya Miaka 35 Dhidi Ya Uturuki
Mnamo Ijumaa, wanajeshi sita wa Uturuki waliuawa na mmoja alijeruhiwa katika shambulio la magaidi kaskazini mwa Iraq.
Akitoa rambirambi zake mnamo Jumamosi juu ya mauaji ya wanajeshi hao, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema kwamba nchi yake itazuia" muundo wa kigaidi" kujitokeza kando ya mipaka yake ya kusini.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun pia alisema kuwa nchi hiyo itaendelea kupigana dhidi ya "aina zote za ugaidi ndani na nje ya mipaka yake kwa uamuzi na ujasiri.”
"Haipaswi kusahaulika kwamba hakuna mashambulizi ya hila yataweza kutingisha umoja na mshikamano wa Uturuki, na mipango ya giza ya magaidi na wadhamini wao hawataweza kushinda mapenzi na uamuzi wa nchi yetu," alisema.
Uturuki ilizindua operesheni ya 'Claw-Lock' mwezi Aprili mwaka jana ili kulenga maficho ya kundi la kigaidi la PKK katika mikoa ya Metina, Zap, na Avasin-Basyan kaskazini mwa Iraq, iliyoko karibu na mpaka wa Uturuki.
Katika kampeni yake ya ugaidi ya zaidi ya miaka 35 dhidi ya Uturuki PKK-iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU - imehusika katika vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, na watoto wachanga.