Shirika la utangazaji la Uturuki la TRT limezindua jukwaa jipya la habari za kidijitali, TRT Afrika, ili kuangazia simulizi za kweli kutoka kwa waafrika wenyewe kwenda kwenye hadhira ya kimataifa duniani kwa lugha nne: Kiswahili, Kiingereza, Kihausa na Kifaransa.
Idhaa hii mpya imezinduliwa moja kwa moja asubuhi ya leo wakati wa siku ya pili ya 'Mkutano wa Kwanza wa Utangazaji' ulioandaliwa na TRT na Umoja wa watangazaji wa Afrika jijini Istanbul. Mkutano huo wa siku tatu ulianza Machi 30.
Sambamba na malengo ya TRT ya uandishi wa habari usio na upendeleo na jumuishi, TRT Afrika itawapa hadhira yake simulizi mbadala kuhusu Afrika na kuangazia taarifa za muhimu zinazo lihusu bara hilo tajiri.
Pia jukwaa hili litaipa sauti Afrika kupitia waafrika walioko ughaibuni, ikiweka mchanganyiko wa kipekee wa maadili yao ya msingi katika moyo wa matukio ya ulimwengu.
Ikiwa na wafanyakazi kutoka nchi 15 katika bara hili, lengo la jukwaa la kidijitali la TRT Afrika ni kuwa chanzo cha habari kinachoaminika katika bara hili, na kuangazia hadithi za kimataifa muhimu kwa hadhira ya Kiafrika na kutoa maudhui ya ubora wa hali ya juu kwa vijana waliounganishwa kimataifa kwenye mitandao ya kijamii.
Inalenga kutoa maudhui ya kipekee ya kidijitali, hadithi za kipekee, uchunguzi na hali halisi ya masuala ya Kiafrika ya ndani kwa watazamaji wa Kiafrika na kimataifa na kukidhi mahitaji ya taarifa kwa Waafrika wanaoishi nje ya nchi na duniani kote.
TRT Afrika itakuwa hai katika nchi nyingi za Afrika kutoka Gambia hadi Morocco, Nigeria hadi Cameroon, Kenya, Tanzania mpaka Afrika Kusini. Kwa njia hii, pia inaongeza kushindilia nia na ahadi ya muda mrefu ya Uturuki kwa bara la Afrika.
TRT Afrika ndiye mwanafamilia mpya kabisa wa TRT inayo jumuisha TRT World, TRT Arabic, TRT Russian, TRT Deutsch, TRT Français na TRT Balkan - zote kibinafsi na kwa pamoja zikileta sauti na mitazamo tofauti kwa hadhira ya kimataifa.