Guler alisema Uturuki inaweka kipaumbele katika kudumisha mazingira ya usalama na utulivu katika Caucasus, pamoja na kutekeleza mara moja miradi ambayo itachangia maendeleo ya eneo hilo. / Picha: AA

Uturuki inajitahidi kuhakikisha amani na utulivu kutoka Bahari Nyeusi hadi Mashariki ya Kati, Ankara imesema.

"Wakati ambapo mvutano na migogoro inaongezeka duniani kote, kama Uturuki, tunafanya jitihada kubwa za amani na utulivu kuwepo kutoka Bahari Nyeusi hadi Afrika, kutoka Mashariki ya Kati hadi Caucasus," alisema Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler. Jumapili wakati wa hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya Ushindi wa Machi 18 wa Canakkale na Wafiadini.

Guler alisema Uturuki imekuwa "mtendaji mzuri" katika kuhakikisha amani ya kimataifa, na utulivu kupitia diplomasia yenye nyanja nyingi chini ya uongozi wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Aliongeza kuwa nchi imekuwa "mwanachama muhimu" wa meza ya mazungumzo na mfumo wa usalama wa kimataifa.

"Badala ya oparesheni ndogo na za muda huko nyuma, leo tunaendesha operesheni endelevu na za kina zinazolenga kutokomeza chanzo cha tishio la ugaidi, kukabiliana na pigo kubwa kwa mashirika ya kigaidi," alisema.

"Kama tusingekuwepo huko sasa, mashambulizi ya mashirika haya dhidi ya nchi yetu na watu wangeendelea ndani ya nchi, kama walivyofanya hapo awali, na utulivu uliopo haungedumishwa," aliongeza waziri huyo.

Guler alisisitiza azma ya Ankara ya kupambana na ugaidi kwa azma na uthabiti kwa ajili ya amani na usalama wa nchi.

TRT World