Erdogan alisisitiza dhamira ya Uturuki ya kuwawajibisha wahalifu wa uhalifu wa kivita huko Palestina. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekosoa historia ya Israel ya ukiukaji wa usitishaji mapigano, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuzuia ukiukaji zaidi wakati wa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kati ya Israel na Hamas.

"Israel, hasa (Waziri Mkuu Benjamin) Netanyahu, ina rekodi kubwa ya ukiukaji wa usitishaji mapigano, hii haipaswi kuruhusiwa wakati huu (huko Gaza)," Erdogan alisema Jumamosi.

Amelaani hujuma ya siku 467 ya Israel huko Gaza ambayo iliua zaidi ya Wapalestina 47,000 na kusema: "Licha ya siku 467 za mauaji ya halaiki na mauaji makubwa, Israel imeshindwa kuvunja irada ya muqawama ya ndugu na dada zetu huko Gaza."

Erdogan alisisitiza dhamira ya Uturuki ya kuwawajibisha wahalifu wa uhalifu wa kivita huko Palestina. “Juhudi zetu za kuwawajibisha wahusika wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu mmoja baada ya mwingine zitaendelea kushika kasi,” alisema.

Uturuki itahamasisha kwa kila njia kuponya majeraha ya Gaza wakati wa usitishaji mapigano, Erdogan aliongeza.

Siku ya Jumatano, Qatar ilitangaza makubaliano ya awamu tatu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la muqawama la Palestina Hamas ili kukomesha zaidi ya miezi 15 ya mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya Gaza, huku usitishaji mapigano ukitarajiwa kuanza Jumapili saa 0630GMT.

Kuhusu Syria, Erdogan alisema "mradi wa Israeli wa kuigawanya Syria katika sehemu tatu, na kuifanya kuwa vipande ambavyo ni rahisi kumeza, umeanguka."

Alisisitiza uungwaji mkono wa Uturuki kwa kurejea kwa wakimbizi kwa hiari huku akipinga urejeshwaji wowote wa kulazimishwa.

TRT World