Viongozi mbalimbali ulimwenguni wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa Uturuki huku benderea zikiendelea kupepea nusu mlingoti nchini Uturuki na ndani ya umoja wa nchi za Kiturk./Picha: Reuters

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umetuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Uturuki, ikionesha mshikamano na jamhuri hiyo kufuatia janga la moto katika hoteli moja huko Bolu ambali pia limegharimu maisha ya watu na kuwaacha wengi na majeraha.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE imetuma salamu hizo kwa watu wa Uturuki na serikali ya nchi hiyo, na pia kwa familia wa waathirika wa tukio hilo, ikiwaombea nafuu ya haraka majeruhi wa ajali hiyo ya moto.

Takribani watu 76 walipoteza maisha na wengine 51 kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mapema Januari 21, katika Jimbo la Bolu.

Viongozi mbalimbali ulimwenguni wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa Uturuki huku benderea zikiendelea kupepea nusu mlingoti nchini Uturuki na ndani ya umoja wa nchi za Kiturk.

TRT Afrika