Kati ya  wapiga kura milioni 64.1 milioni  3.4 wamejisajili kupigia kura nje ya nchi  / Photo: Reuters

Huku wananchi wa Uturuki walio nje ya nchi wakijitayarisha katika uchaguzi wa rais na bunge wa Uturuki, mwangaza sasa uko kwa wapiga kura, ambao watakuwa na sauti ya mwisho katika mchakato wa kidemokrasia.

Kwa miaka mingi, Uturuki imesajili idadi kubwa ya wapiga kura, huku asilimia 86 ya wapiga kura walipiga kura katika uchaguzi wa urais wa 2018.

Wakati watu walio nje ya nchi watapiga kura kati ya Aprili 27 na Mei 9, upigaji kura ndani ya Uturuki utafanyika Mei 14.

Uturuki imepitia mabadiliko makubwa katika mfumo wake wa uchaguzi tangu miaka ya 1990,ikiwemo kuanzishwa kwa uchaguzi wa rais mnamo 2014 na mfumo mpya wa serikali wa 2017.

Na pia sheria mpya ya uchaguzi ambayo ilipitishwa mwezi Aprili 2022 ambayo ilipunguza kiwango cha kura ambayo mgombeaji anahitaji kupata hadi asilimia 7.

Idadi ya Wapiga kura

Ushiriki wa wapiga kura katika uchaguzi wa rais wa Uturuki tangu miaka ya 1990 umekuwa wa juu kiasi, na wastani wa waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 78.5, kulingana na maelezo ya shirika la Kimataifa ya IDEA.

Mwaka 2018 ndiyo ilikuwa kati ya miaka iliyokuwa na wapiga kura wengi zaidi katika historia ya Uturuki, huku 86.2% ya wapiga kura waliotimiza masharti walipiga kura.

Idadi ndogo zaidi ya waliojitokeza kupiga kura ya Uturuki ilikuwa katika uchaguzi wa urais wa 2014, ambapo asilimia 74 ya wapiga kura wanaostahiki walipiga kura zao.

Kulinganisha na demokrasia zingine

Uturuki pia ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha waliojitokeza kupiga kura ikilinganishwa na baadhi ya nchi nyingine za kidemokrasia wakati wa uchaguzi kama - Ugiriki (2019), Marekani (2020), Uingereza (2019), Norway (2021) na India (2019).

Norway ilikuwa na kiwango cha pili cha juu cha waliojitokeza kupiga kura cha asilimia 77 katika uchaguzi wa 2021.

Marekani ilikuwa na asilimia 70.7 ya wapiga kura katika uchaguzi wa 2020, na Uingereza ikiwa na asilimia 67.5 katika uchaguzi wa 2019. Ugiriki ilishuhudia kiwango cha chini kabisa cha wapiga kura waliojitokeza kati ya nchi hizi.

Ni asilimia 57.8 pekee ya wapiga kura wanaostahiki kushiriki katika uchaguzi wa 2019 huku asilimia 67 wakipiga kura zao nchini India katika uchaguzi wa 2019.

Wananchi nje ya nchi watapiga kura kati ya Aprili 27 na Mei 9 huku upigaji kura ndani ya Uturuki utafanyika Mei tarehe 14  

Mabadiliko ya uchaguzi na upigaji kura wa moja kwa moja

Uturuki imefanya chaguzi tano, za mtaa na uchaguzi mkuu, jumla tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa rais mwaka 2014, ambapo rais alichaguliwa na wananchi.

Kabla ya hapo, rais alichaguliwa na bunge, ambalo lilihusisha duru mbili za upigaji kura. Katika awamu ya kwanza, mgombea alihitaji kupata angalau theluthi mbili ya kura katika bunge ili kuchaguliwa.

Iwapo hakuna mgombea aliyepata theluthi mbili ya kura, duru ya pili ya kura ilifanywa kati ya wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi katika duru ya kwanza. Katika duru ya pili, mgombea aliyepata kura nyingi bungeni alichaguliwa kuwa rais.

Rais aliyechaguliwa na bunge alikuwa na uwezo mdogo wa kiutendaji na waziri mkuu aliyeteuliwa na rais kutoka miongoni mwa wabunge wa chama kikubwa zaidi cha bunge alikuwa mkuu wa serikali na alikuwa na mamlaka halisi ya kiutendaji.

Hata hivyo, nafasi ya rais ilibadilika sana kutokana na kura ya maoni ya katiba iliyofanyika mwaka wa 2017, ambayo ilianzisha mfumo mpya wa serikali.

Chini ya mfumo mpya, rais ni mkuu wa nchi na mkuu wa serikali, mwenye mamlaka makubwa ya utendaji.

Rais sasa anachaguliwa moja kwa moja na wananchi kupitia kura ya wananchi kitaifa Wabunge huchaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano.

Siku ya Alhamisi, siku 17 kabla ya uchaguzi muhimu nchini Uturuki, mamia kwa maelfu ya raia wa Uturuki wanaoishi nje ya nchi walianza mchakato wao wa kupiga kura katika nchi wanazoishi au katika vituo vya mpakani vya Uturuki.

TRT Afrika