Uchaguzi Uturuki: Kinyang'anyiro cha Urais chaelekea duru ya pili Mei 28

Uchaguzi Uturuki: Kinyang'anyiro cha Urais chaelekea duru ya pili Mei 28

Zaidi ya watu milioni 64.1 walijiandikisha kupiga kura kumchagua rais, wabunge kwa miaka 5 ijayo.
Marudio ya uchaguzi Uturuki | Picha: AA

Matokeo ya mwisho yanakuja huku zaidi ya asilimia 98 ya kura zikiwa zimehesabiwa kufikia sasa. Rais Erdogan kufikia sasa amepata kura asilimia 49.34 huku Kilicdaroglu akipata kura asilimia 45.00.

Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa saa 2:00 asubuhi (05:00 GMT) na vitafungwa saa 11:00 jioni (14:00 GMT).

Mashirika ya vyombo vya habari yamepigwa marufuku kuripoti matokeo kwa muda hadi marufuku hiyo itakapo ondolewa saa 3:00 usiku (18:00 GMT).

Ikiwa hakuna mgombeaji atakayepata zaidi ya nusu ya kura katika duru ya kwanza ya upigaji kura, duru ya pili ya Mei 28 itafanyika.

Jumla ya masanduku 191,885 ya kupigia kura yameundwa kwa ajili ya wapiga kura nchini.

Kuna kambi tano za vyama vingi zinazoendelea: Muungano wa Watu, Muungano wa Taifa, Muungano wa Ata, Muungano wa Leba na Uhuru, na Muungano wa Kisoshalisti au ujamaa

Fuatilia habari za hivi punde 👇

1241 GMT - Mbio za urais kwenda duru ya pili, YSK atangaza rasmi

Mkuu wa YSK Ahmet Yener ametangaza kuwa uchaguzi wa rais wa Uturuki utafanyika kwa marudio ya kura mnamo Mei 28 baada ya hakuna mgombeaji aliyepata angalau asilimia 50 inayohitajika kushinda wakati wa duru ya kwanza.

“Idadi ya masanduku ya kura za ndani nchini ilifunguliwa kwa asilimia 100, ushiriki ulikuwa asilimia 88.92 na nje ya nchi asilimia 52.69,” alisema.

0345 GMT — Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonyesha asilimia 98.55 ya kura zilizo hesabiwa

• Erdogan: 49.34%

• Ince: 0.43% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 45.00%

• Ogan: 5.23%

0155 GMT — Matokeo ya hivi punde ya urais

Haya hapa ni matokeo ya hivi punde ya urais yanayo onyesha asilimia 98.06 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: asilimia 49.34

• Ince: asilimia 0.43 (imeondolewa)

• Kilicdaroglu: asilimia 44.99

• Ogani: asilimia 5.24

0150 GMT — Matokeo ya hivi punde ya kura za ubunge

Haya hapa ni matokeo ya hivi punde huku asilimia 97.88 ya kura zimehesabiwa:

• Muungano wa Watu: asilimia 49.30

• Muungano wa Taifa: asilimia 35.22

0122 GMT — Uchaguzi uliakisi mapenzi ya taifa: Kurugenzi ya Mawasiliano

Uchaguzi wa rais na bunge wa Uturuki kwa mara nyingine tena ulionyesha nia ya taifa hilo, mkurugenzi wa mawasiliano wa nchi amesema.

Mei 14 kwa mara nyingine tena ilikuwa siku "wakati mapenzi ya taifa hili tukufu" yalipodhihirika, alisema Fahrettin Altun kwenye Twitter.

"Taifa letu limezungumza na kuelekeza njia ya kwenda. Kwa kushiriki katika mshikamano na kwa amani, tutakua pamoja na tutaweka mfano kwa ulimwengu," Altun aliandika.

2355 GMT — Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonesha asilimia 97.23 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 49.36%

• Ince: 0.44 (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 44.96%

• Ogan: 5.25%

2313 GMT - Tuko mbele sana katika uchaguzi: Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema ana "uongozi wa wazi" katika uchaguzi wa Uturuki.

Akiwahutubia wafuasi wake katika makao makuu ya Chama cha AK katika mji mkuu Ankara, alisema kuwa kura za ndani na nje bado zinaendelea kuhesabiwa, akiongeza matokeo ya awali yanaonyesha "tuko mbele sana."

Alisema ameshinda takriban kura milioni 2.6 zaidi ya mshindani wake wa karibu, na kuongeza idadi hiyo itaongezeka katika matokeo ya mwisho.

Erdogan alisema nchi hiyo imekamilisha "sherehe nyingine ya demokrasia" kwa uchaguzi wa Mei 14, akiongeza kuwa nchi hiyo imeshuhudia idadi kubwa ya waliojitokeza kupiga kura katika historia ya taifa hilo.

"Watu waliopiga kura nyingi kwa muungano wetu bungeni, bila shaka wataunga mkono kwa utulivu katika uchaguzi wa urais," Erdogan aliongeza.

2250 GMT — Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonesha asilimia 96.15 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 49.44%

• Ince: 0.44% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 44.86%

• Ogan: 5.26%

2135 GMT — Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonyesha asilimia 94.24 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 49.59%

• Ince: 0.45% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 44.67%

• Ogan: 5.29%

2135 GMT — Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonesha asilimia 94.24 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 49.59%

• Ince: asilimia 0.45 (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 44.67%

• Ogan: 5.29%

2105 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais yanaonesha kuwa asilimia 93.02 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 49.67%

• Ince: 0.45% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 44.59%

• Ogan: 5.29%

2030 GMT - Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonesha asilimia 87.7 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 50.20%

• Ince: 0.48% (imetolewa)

• Kilicdaroglu: 44.02%

• Ogan: 5.30%

2030 GMT - Matokeo ya hivi punde ya urais yanaonesha asilimia 87.7 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 50.20%

• Ince: 0.48% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 44.02%

• Ogan: 5.30%

2030 GMT — Matokeo ya hivi punde ya ubunge yenye asilimia 75.25 ya kura zilizohesabiwa

• Muungano wa Watu: 50.99%

• Muungano wa Kitaifa: 34.25%

2015 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais yanaonesha asilimia 82.54 ya kura zilizohesabiwa

• Erdogan: 50.30%

• Ince: 0.48% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 43.91%

• Ogan: 5.31%

2000 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais yanaonesha kuwa asilimia 89.24 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 50.50 %

• Ince: 0.49 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 43.70 %

• Ogan: 5.31 %

1945 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais yanaonesha asilimia 75.79 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 50.76 %

• Ince: 0.50 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 43.43 %

• Ogan: 5.31 %

1945 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa wabunge kwa hesabu ya asilimia 62.23 ya kura

• Muungano wa Watu: 52.09 %

• Muungano wa Kitaifa: 33.44 %

1930 GMT — Matokeo ya hivi punde ya wa rais yanaonesha asilimia 74.9 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 50.97%

• Ince: 0.50% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 43.22%

• Ogan: 5.31%

1915 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais yanaonesha asilimia 70.4 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 51.23 %

• Ince: 0.51% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 42.95 %

• Ogan: 5.31 %

1915 GMT — Matokeo ya uchaguzi wa wabunge kwa hesabu ya asilimia 49.85 ya kura

• Muungano wa Watu: 53.25% • Muungano wa Kitaifa: 32.59%

1900 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais zinaonesha asilimia 65.7 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 51.44 %

• Ince: 0.51 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 42.73 %

• Ogan: 5.32 %

1845 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais zinaonesha asilimia 60.4 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 51.71 %

• Ince: 0.52 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 42.45 %

• Ogan: 5.32 %

1830 GMT — Omer Celik: Hesabu ya kura ‘inaendelea kwa uwazi’ Msemaji wa chama kinachotawala cha AK Omer Celik amesema kuwa hesabu ya kura inaendelea kwa uwazi. "Utajiri wetu mkubwa ni kuwa na demokrasia inayofanya kazi,’’ amesema Celik, ambaye amedai kuwa msemaji wa muungano wa upinzani na baadhi ya mameya ‘walijaribu kuvuruga data’ zilizotolewa na shirika la Anadolu kabla ya matokeo kukamilishwa. "Tunaheshimu mifumo ya kisheria, shughuli ya kuhesabu na mamlaka ya baraza kuu la uchaguzi (YSK), litakalotangaza matokeo."

1830 GMT — Matokeo ya hivi punde ya rais zinaonesha asilimia 54.8 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 51.96 %

• Ince: 0.53 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 42.19 %

• Ogan: 5.32 %

1830 GMT — Matokeo ya hivi punde ya wabunge kwa hesabu ya asilimia 29.57 ya kura

• Muungano wa Watu: 55.71 %

• Muungano wa Kitaifa: 30.57 %

1815 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais zinaonesha asilimia 47.55 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 52.2 %

• Ince: 0.5 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 41.9 %

• Ogan: 5.3 %

1800 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais zinaonesha asilimia 43.7 ya kura zimehesabiwa • Erdogan: 52.6 %

• Ince: 0.5% (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 41.6 %

• Ogan: 5.4 %

1745 GMT — Matokeo ya hivi punde ya uchaguzi wa rais zinaonesha asilimia 37.9 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 53.02 %

• Ince: 0.56 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 41.04 %

• Ogan: 5.38 %

1745 GMT — Matokeo ya hivi punde ya wabunge

Kura zinahesabiwa za uchaguzi wa bunge nchini Uturuki. Haya ndio matokeo ya hivi punde kwa hesabu za asili mia 13.19 za kura.

• Muungano wa Watu: 60.19 %

• Muungano wa Kitaifa: 26.78 %

1730 GMT — Matokeo ya hivi punde ya kura za rais zinaonesha kuwa asilimia 31.5 ya kura zimehesabiwa

• Erdogan: 53.62 %

• Ince: 0.56 % (amejiondoa)

• Kilicdaroglu: 40.42 %

• Ogan: 5.40 %

1715 GMT — Erdogan anaongoza wakati matokeo ya awali matokeo ya awali yameanza kuingia, huku asilimia 24.7 ya kura zikiwa zimehesabiwa.

• Erdogan: 54.63 % • Ince: 0.56 % (alijiondoa) • Kilicdaroglu: 39.40 % • Ogan: 5.41 %

1635 GMT— Marufuku ya kutangaza matokeo ya uchaguzi yaondolewa

Baraza kuu la uchaguzi nchini Uturuki (YSK) limeondoa marufuku y akutangaza matokeo ya uchaguzi kuanzia 12:30 kwa saa za Uturuki. (15:30 GMT), Mwenyekiti wa YSK Ahmet Yener ameambia waandishi wa habari katika mji mkuu Ankara .

15:00 GMT — Vituo vya kupiga kura vimefungwa

Vituo vya kupiga kura vimefungwa na shughuli ya kuhesabu kura imeanza katika uchaguzi wa rais na wabunge wa Uturuki.

14:22 GMT — Mwenyekiti YSK : "Hakuna hali tete iliyo onekana katika ubao wetu kufikia sasa"

Mwenyekiti wa YSK Yener amesema kuwa utaratibu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa urais na wabunge wa awamu ya 28 umekamilika na kuwa hakuna habari zozote tete zilizo wasilishwa katika ubao wao wa matokeo.

Katika taarifa waliyo andika, Yener amesema kuwa mchunguzi mmoja wa chama na raia wawili walifariki kutokana na mshtuko wa moyo wakati wa shughuli hiyo ya kupiga kura, na ametuma salamu yake ya rambi rambi kwa jamaa waliofariki.

1420 GMT - Erdogan anaondoka Istanbul, kuelekea makao makuu ya chama cha AK

Mwandishi wa TRT World Andrew Hopkins yupo mjini Ankara katika makao makuu ya chama cha AK na anaeleza kuwa hali ipo shwari huku watu wakisubiuri matokeo ya mapema ya hesabu za kura.

Erdogan ameondoka mjini Istanbul na anatarajiwa katika makao hayo makuu ya chama chake muda mfupi ujao,kwa mujibu wa Hopkin.

11:45 GMT - Idadi ya wapigakura inatarajiwa kuvuka kiwango cha juu cha asilimia 90

Mwandishi wa TRT World Mustafa Fatih Yavuz mjini Ankara anasema kuna idadi kubwa ya wapiga kura mjini Ankara na Uturuki kwa ujumla.

Mwaka 1987 waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 93.3 na mwaka 2018 walikuwa asilimia 86.2.

Yavuz anasema idadi ya wapiga kura mwaka huu inatarajiwa kuvuka kiwango cha asilimia 90.

Upigaji kura wa Diaspora pia uliongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2018 hadi asilimia 53 mwaka huu.

1130 GMT - Mpiga kura mwenye umri wa miaka 112 anapiga kura

Gullu Dogan, mkazi mzee zaidi wa Gumushane, mwenye umri wa miaka 112, aliamua kutumia haki yake ya kupiga kura pamoja na watoto wake na wajukuu katika kituo cha kupigia kura cha eneo hilo.

Licha ya kupata urahisi wa kupiga kura yake kupitia kisanduku cha kupigia kura kinachotembezwa, alichagua kuhudhuria uchaguzi huo.

0830 GMT - Sinan Ogan apiga kura

Mgombea Urais wa Muungano wa ATA, Sinan Ogan, alipiga kura mjini Ankara na mkewe Gokcen Ogan. Alitoa wito kwa wananchi kusherehekea pamoja uchaguzi huo.

"Natamani uchaguzi huu ulete ustawi wa nchi yetu na taifa letu. Natoa wito kwa wananchi wetu wote tafadhali tupige kura. Tufanye uchaguzi huu pamoja kama sherehe kwa amani, nina furaha kubwa, namshukuru kila mtu."

0830 GMT - Rais wa Uturuki alipiga kura

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alipiga kura yake katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Uturuki.

“Mchakato wa upigaji kura unaendelea kote nchini bila matatizo yoyote. Wananchi wetu katika eneo lililoathiriwa na matetemeko ya ardhi pia wanapiga kura. Hatukukumbana na matatizo yoyote katika eneo hilo pia,” Erdogan aliwaambia waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake katika wilaya ya Uskudar, jijini Istanbul.

Alisema anataka "mustakhbali mwema kwa nchi yetu na demokrasia ya Uturuki".

0800 GMT - Mgombea wa upinzani Kılıçdaroğlu apiga kura

Mwenyekiti wa chama cha Jamhuri cha (Republican Peoples Party – CHP) ambaye pia ni mgombea wa urais Kemal Kılıçdaroğlu amepiga kura yake katika uchaguzi unaoendelea Uturuki.

Kılıçdaroğlu alipiga kura yake katika shule ya msingi ya Arjantin, mjini Anara.

0500 GMT - Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa Uturuki kwa ajili ya uchaguzi wa urais, ubunge

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa kote Uturuki mapema siku ya Jumapili asubuhi kwa uchaguzi wa rais na wabunge nchini humo.

Rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan anawania muhula wake wa mwisho madarakani, wakati wagombea wa upinzani ni Kemal Kilicdaroglu wa Muungano wa Nation na Sinan Ogan wa Ata Alliance.

Bodi ya Juu ya Uchaguzi (YSK) ilitangaza mapema kwamba zaidi ya raia milioni 64 wanastahili kupiga kura katika uchaguzi wa Mei 14, ikiwa ni pamoja na wapiga kura zaidi ya milioni 3 nje ya nchi.

Upigaji kura utafungwa saa kumi na moja jioni saa za ndani, na matokeo ya kwanza yanatarajiwa kuanza kuja muda mfupi baada ya hapo.

TRT World