Recep Tayyip Erdogan / Photo: AA

Uturuki inajiandaa kwa uchaguzi pacha wa Mei 14 ambao unabeba umuhimu mkubwa sana kwa mustakbali wa nchi hii.

Kwa miaka ishirini iliyopita mtazamo wa kisiasa wa nchi hii umewakilishwa na chama cha Haki na Maendeleo (AK) kikiongozwa na Recep Tayyip Erdogan, ambaye ameshikilia uongozi wa nchi tangu mwaka wa 2002.

Recep Tayyip Erdogan alitajwa kuwa rais wa kwanza wa Uturuki mnamo mwaka wa 2018, kufuatia mabadiliko muhimu ya katiba.

Uturuki imekuwa na mfumo wa bunge tangu kupitishwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka wa 1946 na kwa miongo miwili, tangu mwaka 2002, imeongozwa na serikali za chama kimoja, Chama cha AK, kinachoongozwa na Recep Tayyip Erdogan kimepata ushindi katika chaguzi zote.

Katika miaka yote hii, Uturuki imepiga hatua kubwa kupitia ubunifu wake kuangazia masuala ya ndani na nje ya nchi. Imekuwa ngome ya maendeleo hasa kwa nchi nyingi duniani, na mataifa yaliyokuwa yakigandamizwa na nchi zenye nguvu duniani.

Recep Tayyip Erdogan / Picha : AA

Kwa kuonesha umahiri wake wa kidiplomasia, serikali ya Uturuki imetekeleza jukumu muhimu kuleta maafikiano katika meoneo yanayokumbwa na mizozo kama vile Ukrain na Libya.

Kwa sasa, Uturuki ni ya 19 kati ya mataifa yenye bajeti kubwa zaidi duniani ikiwa na uzalishaji wa ndani wa takriban dola bilioni mia tisa na sita ($906 B). Ni mwanachama wa shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo(OECD), pamoja na shirika la mataifa 20 tajiri zaidi duniani (G20), na inaendelea kuwa mfadhili mkuu rasmi wa misada ya maendeleo.

Kati ya mwaka wa 2006 na 2017, chini ya uongozi wa rais Recep Tayyip Erdogan, nchi hii imefanya mabadiliko makubwa na kufikia viwango vya juu vya ukuaji ulioiwezesha kupata hadhi ya kiwango cha pato la juu na kati, na kupunguza umaskini kwa takriban nusu kwa kufikisha asili mia 9.8 ya raia ambao wanaishi kwa chini ya dola $6.85 kwa siku kufikia mwaka 2020.

Uturuki inajivunia kuwa na mtandao wa tano kwa ukubwa duniani wa kidiplomasia ikiwa na mabalozi 260 za kigeni.

Mabadiliko ya mwaka 2017 ya Uturuki kwenda kwa mfumo wa urais, ulileta mabadiliko makubwa katika siasa za kitaifa na kusababisha kuundwa kwa vyama viwili vya muungano.

Mojawapo kinaitwa People's Alliance, kikiongozwa na chama cha AK na ndani yake kuna vyama vya vuguvugu la kitaifa (MHP), chama cha muungano mkuu (BBP) na chama kipya cha maslahi (Yeniden Refah).

Mbabadiliko katika mfumo wa uchaguzi wa 2017 yalisababisha kuundwa kwa vyama vya muungano kabla ya uchaguzi, ambayo yamegeuza taswira ya kisiasa ya  Uturuki / Picha : AA

Muungano mwingine unajulikana kama Muungano wa taifa (Nation Alliance), na unaongozwa na chama kikuu cha upinzani kinachoegemea mrengo wa kushoto ya kati, Chama cha Jamhuri (CHP). Pia unajumuisha vyama vya IYI , kinachoegemea mrengo wa kulia na kupigania uzalendo pamoja na vyama vya Saadet na kile cha Demokrasia , vilivyo na idadi ndogo ya wapiga kura.

Sasa miungano hiyo inajiandaa kwa ushindani mkubwa wa urais wa Uturuki mwaka wa 2023. Recep Tayyip Erdogan atawania muhula wa pili kama mgombea kinara wa chama tawala cha AK. Mpinzani wake mkuu atakuwa Kemal Kilicdaroglu ambaye chama chake cha CHP kipo katika muungano wa Kitaifa kwa ajili ya uchaguzi wa 2023.

Anafuatiwa na Sinan Ogan, mwana zuoni aliye na asili ya Azerbaijan na Uturuki, ambaye pia anawania kwa titiki ya chama cha Muungano wa kitaifa kwa ajili ya uchaguzi wa mwezi Mei, na mgombea wa chama cha Memleket Muharrema Ince kama mgombea wa nne katika uchaguzi wa Uturuki 2023.

Kwa kuwa chama cha AK kimekuwa uongozini kwa miongo miwili na kimeifikisha Uturuki viwango vya juu katika ngazi ya kimataifa kutokana na ufanisi wake katika nyanja mbali mbali, uchaguzi huu wa 2023 unatazamiwa kuwa muhimu zaidi kwake kuweza kuendeleza maono yake ya nchi.

Tuangazie baadhi ya ufanisi mkubwa wa Uturuki katika miongo miwili iliyopita pamoja na ahadi zake katika uchaguzi mkuu ujao.

Teknolojia ya hali ya juu katika sekta ya ulinzi

Punde baada ya Erdogan kushikilia wadhifa wa uongozi kama waziri mkuu mwaka wa 2003, alianzisha mara moja mabadiliko katika uchumi, soko la wafanyakazi, viwanda vya uzalishaji akiwa na malengo muhimu katika ulinzi na sekta nyingine zilizobainika kuwa muhimu sana katika ukuaji wa taifa wa Uturuki.

Tangu wakati huo, Uturuki imeweza kuweka sera thabiti za uzalishaji na kupunguza kutegemea uagizaji wa bidhaa za nje huku ikilenga kuimarisha uzalishaji wa ndani, hasa katika sekta za ulinzi na utengenezaji magari.

Uturuki ilitengeneza ndege zisizo na rubani kwa lengo la kusitisha kutegemea kuagiza kutoka nje hasa katika nyanja za Ulinzi, viwanda na teknolojia / Picha AA

Katika miongo miwili sekta ya ulinzi ya Uturuki ilipunguza utegemeaji wa kigeni kutoka asilimia 80 hadi 20.

Huku washika dau zaidi wakijiunga na juhudi hizi, kiwanda hicho kimeweza kupanuka, kikiwa sasa na makampuni zaidi 1500 yanayohusika na masuala ya ulinzi, ikilinganishwa na 26 pekee yaliyokuwepo mwaka wa 2002 na yakifanya miradi 750 kwa mpigo.

Isitoshe, bajeti ya Uturuki ya miradi ya ulinzi ilikuwa $5.5 bilioni mwaka wa 2002. Na sasa imefikia ukubwa wa $75 bilioni wa miradi mbali mbali, ikiwemo ile iliyotajwa na rais Recep Tayyip Erdogan katika hotuba yake hivi karibuni kuwa inashindaniwa katika zabuni.

Mnamo mwaka wa 2022, Uturuki ilifikia kuuza nje vifaa vya ulinzi vya thamani ya zaidi ya dola $3 billioni na huenda ikakaribia dola $4 billioni kufikia mwisho wa mwaka huu, na kufikisha viwango vya mauzo ya nje ya nchi kulingana na baadhi ya mataifa ya ulaya katika jumla ya mauzo yao ya vifaa vya ulinzi.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema mwezi Oktoba, kuwa vyombo visivyokuwa na rubani vya Uturuki (UAV) vimeleta mabadiliko makubwa katika vita vya kisasa.

Ndege isiyokuwa na rubani ya (UAV) ilitua salama kufuatia juhudi za muda mrefu za kiwanda cha ulinzi cha uturuki na ni hatu anyingine katika kuimarisha kiwanda cha ulinzi cha uturuki kilicho na nembo ya taifa / Picha : AA

Mojawapo ya kampuni kubwa ya kibinafsi ya vifaa vya kivita, Baykar, imezindua hivi karibuni ndege ya kivita isiyokuwa na rubani, Bayraktar Kizilelma, au Tufaha Nyekundu, iliyomiminiwa sifa tele kutoka kote duniani.

Baada ya kumaliza safari yake ya kwanza mnamo Disemba mwaka jana, Kizilelma inawakilisha upanuzi mkubwa na uwezo wa ndege zisizo na rubani kufanya upelelezi na kubeba makombora.

Ndege hiyo isiyokuwa na wafanyakazi wowote inatarajiwa kufanya shughuli nyingi za kijeshi kama vile mashabulio ya kimkakati, kukazia kinga za angani za adui na kuangamiza kinga za angani za adui.

Kifaru aina ya Altay ni uvumbuzi mwingine, ambapo ni aina ya chombo cha Uturuki kilicho lenga kuimarisha vikosi vya jeshi katika viwango vya kisasa.

Kifaru cha Altay ni moajwapo ya miradi iliyotekelezwa chini ya uongozi wa rais Recep Tayyip Erdogan ili kuimarisha kiwanda cha kijeshi na majeshi ya Uturuki / Picha : AA

Kifaru hicho kimebeba bunduki kuu ya Rheinmetall ya 120mm, na bunduki ndogo ya rashasha ya 7.62mm.

Inanuiwa kutumiwa kuongeza usalama kwa vifaru vingine na vyombo vilivyo na kinga dhidi ya mashambulio mbali mbali ya kama vile makombora ya kulenga vifaru, maguruneti ya kurushwa kwa roketi na silaha zingine zozote.

Kilele cha uvumbuzi wote huu katika kiwanda cha ulinzi cha Uturuki, ni ndege ya TCG-Anadolu, ambacho ni chombo cha kwanza duniani cha kusafirishia ndege za kivita zisizokuwa na rubani (UCAV) na kubwa zaidi ambayo imewahi kutengenezwa na uturuki.

TCG-Anadolu ni ya kipekee kwa njia nyingi na itaimarisha nguvu za jeshi la Uturuki, itaweza kufanya oparesheni za vyombo vingine kama vile ndege za kivita zisizokuwa na rubani za Bayraktar TB-3, Akinci na Kizilelma pamoja na ndege nyepesi ya kivita ya Hurjet.

Ndoto ya Uturuki ya miaka 60

TOGG ni gari la umeme la kwanza la Uturuki na ishara ya maendeleo makubwa ya teknolojia ya nchi.

Kundi la pamoja la makampuni ya kutengeneza magari ya Uturuki, linaotumia jina TOGG, lilitangaza mfano wa kwanza wa gari la kielektroniki mnamo Disemba 2019. Sasa Uturuki inalenga kutengeneza magari milioni moja katika mitindo mitano tofauti kufikia mwaka 2030.

Uzinduzi wa gari salama kwa mazingira ya TOGG, lilitarajiwa pakubwa katika historia ya Uturuki, ikiashiria maendeleo makubwa ya teknolojia nchini / Picha AA

TOGG imekuwa gari la kwanza la Uturuki kupokea tuzo ya iF ya ubunifu wa mitindo mwaka wa 2021, mojawapo ya matuzo ya hadhi ya juu zaidi duniani ya ubunifu katika magari aina ya SUV.

Makampuni ya dunia yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza magari ya umeme cha Uturuki, amesema rais Recep Tayyip Erdogan wakati wa hafla ya uzinduzi wa TOGG na kuongeza kuwa kupitia ushirikiano na wizara ya viwanda na teknolojia, serikali imeanzisha mradi wa ku ezeka vituo zaidi ya 1500 vya kuchaji kwa kasi gari hizo, katika mikoa yote 81 nchini.

Ugunduzi wa gesi katika Bahari Nyeusi

Uturuki imepampu gesi ya kwanza asilia iliyozalishwa kutoka Bahari Nyeusi hadi kwa hifadhi yake ya kitaifa, hatua itakayoiwezesha kuendelea kujitegemea kwa kawi.

Kabla ya uchaguzi wa Mei 4, wakati wa hafla ya uzinduzi katika mji wa Zonguldak, rais Recep Tayyip Erdogan alitangaza kuwa nyumba zote zitapokea gesi bila malipo kwa muda wa mwezi mmoja kama maadhimisho ya uzinduzi huo, na hivyo kuzipunguzia familia gharama ya takriban lira 625 lira ($32.2).

Inaaminiwa kuwa gesi inayozalishwa ndani ya nchi na gesi iliyogunduliwa katika Bahari Nyeusi itapunguza utegemeaji wa Uturuki wa kawi pamoja na muimarisha himaya ya bahari zake

Katika miongo miwili iliyopita, Uturuki imepata maendeleo makubwa katika sekta hii.

Kampuni ya Petroli ya Uturuki (TPAO), inayomilikiwa na serikali ambayo inazalisha mafuta na gesi, imetangaza kukamilika kwa bomba linalopitisha gesi kutoka Bahari Nyeusi hadi ufuoni.

Kuongeza pia, mita bilioni 58 za ujazo za gesi ziligunduliwa mwezi Disemba katika kisima cha Caycuma-1 kusini magharibiu mwa Bahari Nyeusi.

Uturuki itaweza kukidhi takriban asili mia 30 ya mahitaji yake ya gesi asilia kutoka kwa hifadhi za Bahari Nyeusi baada ya uzaishaji kufikia kilele na itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa taifa wa uagizaji gesi kutoka nje.

Takriban mita za ujazo 25 za gesi kwa mwezi zitaondolewa kutoka kwenye malipo ya gesi kwa muda wa mwaka mmoja na utumiaji wa gesi asilia utakuwa bure kwa raia kwa muda wa mwezi mmoja kama juhudi za kuwalinda dhidi ya gharama ya kawi inayoendelea kupanda.

Ukaguzi huru umeonesha kuwa hifadhi za gesi za taifa zitafikia bilioni 710 mita za ujazo kufikia mwishoni mwa 2022, zikiwa na thamani ya soko la kimataifa ya $1 trilioni.

Msaada kwa mamilioni

Mpango mwingine ulioanzishwa na serikali ya Erdogan katika miongo miwili iliyopita ni kuondolewa kwa umri wa kustaafu.

Mpango huo mpya unawafaidi wale walioanza ajira kabla ya Septemba 1999 pale sheria inayodhibiti muda wa kustaafu ilipobadilishwa, na wale waliohitimu miaka 20-25 katika ajira zinazohusisha usalama wa jamii.

Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, umri wa chini zaidi unaohitajika kwa mtu kustaafu, - 58 kwa wanawake na 60 kwa wanaume- umeondolewa, na hivyo kuwawezesha zaidi ya wafanyakazi milioni 2 kustaafu mapema.

Wapinzani wakuu na Manifesto

Huku rais Recep Tayyip Erdogan na chama chake cha Haki na Maendeleo AK, wakimulika mafanikio yao makubwa katika miaka 20 iliyopita, vyama vya upinzani pia vimekuwa vikitoa ahadi zao za kampeni, kama vile kuwezesha usafiri wa raia wa uturuki bila vibali katika nchi za Ulaya, wakitaka kuwavutia wapiga kura.

Rais Recep Tayyip Erdogan ametangaza manifesto ya chama cha Haki na Maendeleo AK, kabla ya uchaguzi wa 2023 wa urais na wabunge.

Manifesto hiyo iliyo na mada 23, inalenga kuponya kidonda cha tetemeko la ardhi la mwezi Februari, kujenga upya miji katika mikoa 11, na kuunda nafasi milioni 6 mpya za ajira katika miaka mitano ijayo ili kupunguza ukosefu wa ajira hadi asili mia 7.

Recep Tayyip Erdogan pia ameahidi kupeleka kwa kas/

i uwekezaji na ukuzaji wa utalii nchini kwa lengo la kupata zaidi ya watalii milioni 90 na kukusanya $100 billioni kama pato kutoka kwa utalii. Manifesto hiyo pia ilihusisha maeneo mengine ya uchumi na mazingira.

Recep Tayyip Erdogan aliapa kuzidisha nguvu za Uturuki katika kawi, kilimo, elimu na usafiri, na kuwa atajenga ‘’kitovu cha Uturuki’’ na sera ya kigeni ya amani na uthabiti.

Erdoan

Namna uchaguzi unavyofanywa nchini Uturuki

May 14, raia wa Uturuki watapiga kura kumchagua rais na wabunge. Wengi wanauona uchaguzi kuwa kuwa wa kihistoria.

Rais wa Uturuki anachaguliwa kupitia mfumo wa upigaji kura wa raundi mbili, ambapo mgombea anatakiwa kupata ushindi bayana kabisa wa kura nyingi zaidi au kupata wingi wa zaidi ya asili mia 50 za kura zote kitaifa.

Uchaguzi wa Urais

Watu wanne wameweza kukusanya saini 100,000 zinazohitajika kuidhinishwa kama wagombea wa urais wa Uturuki 2023.

Iwapo hakuna mgombea atakayepata wingi wa kura unaohitajika katika awamu ya kwanza, basi raundi ya pili ya upigaji kura itafanyika Mei 28 kwa uchaguzi wa Uturuki 2023.

Matokeo ya kitaifa yanatangazwa na baraza kuu la uchaguzi (YSK) baada ya kuhesabiwa kura zote.

Turkish elections

Idadi kubwa zaidi ya raia wa Uturuki wanaopigia kura ughaibuni wapo magharibi mwa Ulaya, ambako wafanyakazi wa Uturuki walihamishwa baada ya vita vya pili vya kidunia miaka ya 1960, katika mpango wa wakati huo wa kujenga upya. Wanawakilisha idadi kubwa zaidi ya waislamu wahamiaji walioko magharini mwa Ulaya.

Upigaji kura ughaibuni unafanyika kati ya Aprili 27 hadi Mei 9, huku upigaji kura nchini Uturuki ukifanyika tarehe 14 Mei.

TRT Afrika