Na Ibrahim Karatas
Anadolu ina umbali wa maili 9.000 za baharini na inaweza kusafiri kwa kasi ya juu ya fundo 21 ikiwa imebeba UCAV 41 au helikopta 29 (UCAV 11 au helikopta 10 katika sitaha ya ndege ya mita za mraba 5.440 na UCAV 30 au helikopta 19 kwenye hangar maalumu. Pamoja na wanajeshi 1,223.
Vinginevyo, inaweza kusafirisha magari 27 yenye silaha na mizinga kuu 30 ya vita. Meli pia inaweza kutumika kama kituo cha hospitali wakati wa shida.
TCG-Anadolu awali ilijengwa kama Kituo cha Kutua cha Jukwaa (LHD) ambapo Jeshi la Wanamaji la Uturuki lilipanga kupeleka helikopta na ndege za kivita. Mpango huo ulirekebishwa na wahandisi wa Kituruki kisha kuubadilisha kuwa yakubeba UCAV, ya kwanza katika historia ya jeshi la wanamaji.
Anadolu itaweza kufanya shughuli zake na ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB-3, Akinci na Kizilelma pamoja na ndege nyepesi ya kijeshi Hurjet. Safari ya kwanza ya TB-3 itatokea mapema 2024.
TCG-Anadolu ni ya kipekee katika nyanja nyingi na itaongeza nguvu kwa jeshi la Uturuki. Kitaalam, ingawa ina muundo sawa na meli ya Uhispania Juan Carlos I, uwezo wake wa kurusha ndege zisizo na rubani na ndege nyepesi za kivita, huipeleka meli hiyo hadi ngazi ya juu.
Kujiamini na ujasiri
Ingawa LHD sawa zimeundwa kwa ajili ya kutua kwa helikopta, kwenye Anadolu, sio tu ndege zinazopaa wima lakini zile zinazohitaji njia fupi za kuruka zinaweza kufanya kazi ndani yake.
Ubainifu huu umewahamasisha wanamaji wengine, huku Wamarekani, Wachina na Wajapani wakiripotiwa kupanga kupata meli zinazo fanana.
Iwapo watafuata hatua za jeshi la Uturuki, basi Uturuki itaanzisha dhana mpya labda ya kwanza kabisa katika ulimwengu wa wanamaji.
Meli ya kivita inatoa imani na ujasiri kwa meli za Uturuki na serikali kuunda meli kubwa kama hizo.
Rais Erdogan tayari alisema kwamba wataanza uzalishaji wa shehena kubwa yakubeba ndege.
Ingawa kampuni ya Uhispania ya Navantia ilitoa ilichangia katika teknolojia, kama vile muundo na vifaa muhimu kwa TCG-Anadolu, meli kubwa zinazo fuata zitazalishwa kiasili.
Kwa matokeo haya, moja ya faida muhimu zaidi kwa Uturuki ni teknolojia ya kuunda meli kama hizo. Wazalishaji wa Kituruki pengine watajenga kwa ajili ya wateja wa kigeni na kubadilisha uzoefu wao kuwa mapato pia.
Njia za kutengeneza
Zaidi ya hayo, jeshi la Uturuki litaweza kutumia vyema baadhi ya ndege zake katika orodha ya vikosi vya anga kwenye jukwaa la majini.
Hii ina maana kwamba badala ya kushambulia adui kwa meli hiyo ya kivita, ndege zisizo na rubani zitapaa kutoka kwenye meli ya Anadolu ambayo sasa ni kituo na kupaa hadi kilomita 1000 kutoka ilipo meli.
Zaidi ya hayo, kando na kushambulia adui wakati ikitia nanga, meli hiyo pia inapanua safu ya ndege zisizo na rubani kwa kuwa kituo cha anga baharini.
Anadolu pia itawezesha shughuli katika maeneo ya mbali. Kwa mfano, kama ingekuwa katika orodha wakati wa operesheni ya kijeshi ya jeshi la Uturuki nchini Libya, matokeo yangeweza kuwa ya haraka na yenye ufanisi zaidi
Ikizungukwa na bahari tatu, vitisho vikubwa kwa usalama wa Uturuki huenda vikatoka baharini. Kadiri jeshi la wanamaji linavyokuwa na nguvu, ndivyo inavyozuia zaidi.
TCG-Anadolu itahamisha askari, silaha, ndege, makombora, nk, kutoka bahari moja hadi nyingine kwa kiasi kikubwa na kwa gharama ndogo.
Kulingana na michango iliyo hapo juu kwa jeshi la Uturuki, meli hiyo mpya kabisa itafungua njia kwa manufaa ya kisiasa, pia.
Silaha kubwa kuliko zote
Kwanza, uwezo wa kuhamisha wanajeshi na silaha kwa wingi vinawezekana sasa, Uturuki inaimarisha msimamo wake wa kikanda.
TCG-Anadolu ni kama kituo cha jeshi kinachotembea ambacho kinaweza kutiwa nanga kwenye bahari yoyote. Mtu anaweza kuiona karibu na mwambao wa Libya au Bahari ya Shamu au Baltic.
Onyesho kama hilo la nguvu litatoa imani kwa marafiki na washirika (kama vile walio katika NATO) wa Uturuki huku likisababisha wasiwasi katika miji mikuu ya wapinzani.
Inaweza hata kuwalazimisha wale wanaogombana na Uturuki kutatua matatizo yao kwa amani. Kwa maneno mengine, Anadolu, chombo cha nguvu ngumu, kinaweza kutoa mazingira mapya ya kumaliza migogoro.
Kwa ujumla, TCG-Anadolu ndiyo silaha kubwa zaidi ambayo Uturuki imewahi kutengeneza, na itakuwa na matokeo kisiasa, kiuchumi na kikanda.
Inathibitisha kuwa miradi mikubwa iliyojengwa kwa wakati ufaao kwa mahitaji sahihi huongeza heshima ya kiongozi na nchi, bila kusahau michango mingine.
TCG-Anadolu sio tu mradi wa kijeshi lakini pia mnara mkubwa unaoonyesha nia ya Uturuki, shauku na mipango ya siku zijazo.
Mwandishi, Dk Ibrahim Karatas, ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanahabari aliyebobea katika masuala ya sera za kigeni za Uturuki, Mashariki ya Kati na usalama.