Recep Tayyip Erdogan: Mgombea urais wa chama cha People’s Alliance Uturuki

Recep Tayyip Erdogan: Mgombea urais wa chama cha People’s Alliance Uturuki

Erdogan hajapoteza uchaguzi tangu 1994. Haya ndiyo yamemfanya asishindwe kisiasa
Recep Tayyip Erdogan / Photo: AA

Uturuki inaelekea kwenye uchaguzi mkuu katikati ya mwezi Mei .

Ambapo Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mwenye umri wa miaka 69 atakutana katika debe ya kura na na mgombea urais wa muungano wa vyama vya upinzani.

Tangu achaguliwe kuwa meya wa Istanbul mnamo 1994, Recep Tayyip Erdogan hajapoteza uchaguzi hata mmoja dhidi ya mpinzani yeyote. Katika maisha yake yote, ameshindwa mara mbili pekee - wakati wa kampeni zake mbili za kwanza - katika miaka ya 1980.

Mnamo Mei 14, wakati uchaguzi wa urais na ubunge utafanyika, Recep Tayyip Erdogan - ambaye alishinda chaguzi mbili za awali za 2014 na 2018 - anaomba kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Uturuki kwa muhula mwingine.

Anaungwa mkono na chama cha People's Alliance, muungano wa kisiasa wa Chama cha Haki na Maendeleo, yaani Justice and Development Party (AK Party), chama cha Nationalist Movement Party (MHP), BBP, Yeniden Refah Party na HUDA PAR.

Kuibuka kwa chama cha AK na dira ya kisiasa ya Recep Tayyip Erdogan

Recep Tayyip Erdogan na wafuasi wake walianzisha Chama cha AK kwa msingi wa msimamo wa kidemokrasia wa kihafidhina mwaka 2001, na mwaka uliofuata, chama hicho kilidai wingi wa wabunge katika ushindi mkubwa ambao haukutarajiwa dhidi ya vyama vya jadi vya kulia na kushoto vya Uturuki, na kufungua njia, kwa mtindo mpya wa kisiasa chini ya uongozi wa Recep Tayyip Erdogan.

Mnamo 2002, wachambuzi wachache walidhani kwamba Recep Tayyip Erdogan na Chama chake cha AK wangepata ushindi wa nguvu, na si tu kupata nguvu za kutosha za kisiasa kubadilisha mfumo wa bunge la nchi hiyo kuwa mfano wa rais katika kura ya maoni muhimu iliyofanyika mwaka 2017.

Lakini, Recep Tayyip Erdogan, tangu siku ya kwanza, amefuata malengo yake ya kisiasa bila kuchoka, kuunda nchi ambayo inaweza kuwekeza katika bara la Afrika na kuchukua nafasi muhimu katika migogoro tofauti kutoka Ukraine hadi Azerbaijan, Libya, na Syria, kuboresha kwa kiasi kikubwa usalama na nishati ya Uturuki.

Tofauti na viongozi wengi wa kisiasa wa Magharibi ambao wanadaiwa kupanda kwa vyeo kwa miundo ya kisiasa ya kidemokrasia inayozingatia wasomi, Recep Tayyip Erdogan yeye ameanzia kutoka chini na mwenye asili ya unyenyekevu.

Anatoka pembezoni mwa Uturuki ambapo ukandamizaji wa udini na uhafidhina chini ya awamu ya Kemalist ulienea kwa muda mrefu.

Rais Erdogan anawakilisha chama cha People's Alliance ambacho ni muungano wa vyama vya (MHP), BBP, Yeniden Refah na HUDA PAR

Baba yake Recep Tayyip Erdogan alitoka Guneysu, wilaya ya milimani katika mkoa wa Bahari Nyeusi wa Rize, ambako alihudumu kama nahodha wa kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Uturuki.

Recep Tayyip Erdogan alizaliwa na kukulia katika wilaya ya Kasimpasa iliyopo Istanbul.

Iko katika Pembe ya Dhahabu ya Istanbul (Halic), Kasimpasa kwa muda mrefu imekuwa wilaya ya shughuli nyingi .

Recep Tayyip Erdogan aliuza limau na simiti barabarani, akipata ufahamu wa kina wa uzoefu wa raia wa kawaida wa Uturuki na kujihusisha na maisha ya mijini, ambapo hisia za kihafidhina na za utaifa zilichanganyikana na hamu ya maisha mashuhuri ya Ottoman ya zamani.

Katika umri mdogo, Recep Tayyip Erdogan alipendezwa na mpira wa miguu na siasa. Alikaribia kuchezea Fenerbahce, kilabu cha kandanda kinacho ongoza soka la Istanbul, lakini baba yake alipinga tamaa ya michezo ya mwanawe hivyo Recep Tayyip Erdogan akachagua taaluma ya siasa.

Recep Tayyip Erdogan alihitimu na shahada ya Utawala wa Biashara, mwaka 1981 kutoka katika Chuo cha Uchumi na Sayansi ya Biashara cha Istanbul, ambacho baadaye kiliitwa Kitivo cha Uchumi na Sayansi ya Utawala cha Chuo Kikuu cha Marmara.

Rais Erdogan alifika wakati muhimu katika safari yake ya kisiasa  mwaka wa 1994 baada ya kuwa meya wa Istanbul /Source AA

Jukumu la vuguvugu ya Milli Gorus kwenye Fikra za Kisiasa za Recep Tayyip Erdogan

Recep Tayyip Erdogan alijiunga na vuguvugu la Milli Gorus (Maono ya Kitaifa), ambalo kwa sehemu kubwa lilikuwa limeanzishwa na Necmettin Erbakan, mhandisi wa Kituruki na mwenye imani kali za kidini. Erbakan na marafiki zake walianzisha chama cha National Salvation Party (MSP) mwaka 1972 kama mrengo wa kisiasa wa Milli Gorus.

Ajenda ya kisiasa ya vuguvugu la Milli Gorus ilitokana na imani kwamba, kama nchi yenye Waislamu wengi, Uturuki inaweza, kupitia mkakati wa maendeleo ya kiuchumi ulioanzishwa juu ya roho ya kihafidhina ya ujasiriamali wa Anatolia, kuwa nguvu kubwa bila kuathiri maadili yake ya msingi ya Kiislamu.

Mnamo mwaka 1976, Recep Tayyip Erdogan alikua kiongozi wa vijana wa chama cha ‘National Salvation Party’ wilaya ya Beyoglu, ambayo, wakati huo, ilijumuisha kitongoji chake cha Kasimpasa. Muda mfupi baadaye, akawa mkuu wa tawi la vijana la Istanbul la chama.

Kufuatia mapinduzi ya kikatili ya kijeshi ya 1980 yaliyoteka Uturuki, Recep Tayyip Erdogan aliendelea kufuata njia ya Erbakan, na kuwa mwenyekiti wa tawi la Istanbul la Chama kipya cha Wekfare Party , mnamo 1985. Baada ya majaribio mawili ya kutofanikiwa kuwa meya wa Beyoglu na Mbunge wa Chama cha Ustawi Istanbul, hatimaye alifikia hatua muhimu katika taaluma yake ya kisiasa mnamo 1994.

Meya wa Istanbul dhidi ya uongozi wa kijeshi

Wakati Recep Tayyip Erdogan alipogombea wadhifa katika uchaguzi wa manispaa ya mji mkuu wa Istanbul dhidi ya wagombea mashuhuri, wagombea wengi walipuuza ombi lake, wakidhani kwamba hakuna njia yoyote mgombea wa Chama cha Welfare Party angeweza kushinda.

Hata alipuuzwa na watangazaji kadhaa wakuu wa vyombo vya habari wa vipindi vya mazungumzo ya kisiasa, ambao walikataa kumwalika kwenye vipindi vyao, wakiamini kwamba hakuwa na uwezo wa kushinda.

Lakini asubuhi ya Machi 27, aliibuka mshindi na kushitua taasisi inayoongozwa na jeshi la nchi hiyo, ambayo iliona Chama cha Welfare Party, (RP) kama tishio la kiitikadi kwa tafsiri yao kali kwa kauli yao ya uongozi mkali, ambayo ilipiga marufuku hata hijabu katika vyuo vikuu wakati huo.

Katika kazi yake ya kisiasa, Rais Recep Tayyip Erdogan aliongoza miradi kwa ufanisi katika sekta za usafiri, nishati, na viwanda vya usalama  Picha: AA

Alionyesha ustadi wake wakati wa utawala wake akiwa meya, akirekebisha shida kadhaa kuu za jiji, pamoja na kukatwa kwa maji, shida za usafirishaji, kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira na usimamizi wa taka, ambayo ilisababisha mlipuko wa gesi ya methane katika wilaya ya Umraniye upande wa Asia wa Istanbul, mnamo 1993 chini ya meya wa hapo awali.

Pia aliongoza mradi uliofaulu wa kusafisha Pembe ya Dhahabu, ambayo maji yake yanapakana na kitongoji chake kipenzi cha Kasimpasa.

Kanuni ya kutenga mwonekano wa kidini kutoka kwa umma na kufungwa kwa Tayyip Erdogan

Lakini mafanikio ya manispaa ya Recep Tayyip Erdogan haikujalisha uongozi mkuu wa wakati huo wenye itikadi kali uliochochewa na Ufaransa, ambao ulitetea utawala wa serikali juu ya hisia za kidini, kinyume na itikadi za uingereza ambazo zilitetea mgawanyiko wa wastani wa dini na serikali.

Mnamo 1999, Recep Tayyip Erdogan alihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwasababu ya kukariri shairi lililoandikwa na mwandishi mzalendo, Ziya Gokalp, ambaye mawazo yake yalikuwa msukumo mkubwa kwa mwanzilishi wa Uturuki, Mustafa Kemal Ataturk.

Hukumu hiyo yenye utata pia ilisababisha kupigwa kwake marufuku kisiasa, na kumlazimu Recep Tayyip Erdogan kuacha nafasi yake ya umeya.

Ingawa hukumu hiyo ilikuja kama mshtuko mkubwa kwa raia wa kihafidhina na watu wengi wa Istanbul, ambao waliona maisha yao yakiboreshwa kwa kiasi kikubwa chini ya uongozi wa Recep Tayyip Erdogan, ilisababisha kuamka kwa kiongozi wa baadaye wa Uturuki.

Mnamo 2013, akiwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Erdogan alitembelea tena gereza la Pinarhisar, lililoko Kirklareli, mkoa wa Uturuki eneo la Ulaya la Thrace, ambapo alikuwa amefungwa, akisema, "Kwangu mimi, Pinarhisar ni ishara ya kuzaliwa upya, ambapo tulitayarisha kuanzishwa kwa Chama cha Justice and Development Party (AK Party). Hapo ndipo tulipochukua hatua ya kwanza kuelekea kuanzisha Uturuki mpya na kubwa.”

Hukumu ya kisiasa ya rais Recep Tayyip Erdogan na wasomi watawala wasio na msimamo mnamo 1999 ilitengeneza maono yake ya kisiasa ya Uturuki mpya na kubwa' na kuzaa Chama cha AK / Picha: AA

Kiongozi wa Uturuki: Kukubalika na wapiga kura wote wa mrengo wa kati wa kulia, wa kitaifa na mrengo wa kushoto

Miaka miwili baada ya kuachiliwa kutoka kwa Pinarhisar, Recep Tayyip Erdogan na wenzake wenye nia kama hiyo, ambao waliitwa "wanamageuzi" - kinyume na wafuasi wa kikundi cha Erbakan, ambao walijulikana kama "wana mila" - walianzisha Chama cha AK baada ya mgawanyiko katika Chama cha Maadili, mrithi wa Chama cha Welfare Party kilichopigwa marufuku.

Kupitia kwa Chama cha AK, Recep Tayyip Erdogan alilenga kuwavutia wapiga kura wa mrengo wa kati na wa kitaifa, na vile vile wapiga kura wa mrengo wa kati wa mrengo wa kushoto waliokuwa wanahama kutoka msimamo wa Erbakan wa Milli Gorus.

Lakini aliendelea kuheshimu mapambano ya Erbakan hadi kifo chake, akisifu urithi wake.

Mafanikio ya Uchaguzi: Ushindi wa uchaguzi miaka ya 2002, 2007, 2011, 2014 na 2018

Uchaguzi mkuu wa 2002

Mnamo 2002, mkakati wake mpya ulionekana kuwa uvumbuzi mkubwa wa kisiasa baada ya chama chake kuingia madarakani, kikishinda vyama vya jadi vya nchi - na kwa kura nyingi, kikichukua viti 362 kati ya 550. Katika kipindi hiki, mageuzi mengi ya kidemokrasia yamepitishwa chini ya uongozi wake, kuruhusu matangazo ya lugha ya Kikurdi hadharani ambayo yamekuwa mwiko kwa muda mrefu.

Tangu wakati huo, Recep Tayyip Erdogan ameshinda uchaguzi mara mbili kuu za kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo mnamo 2007 na 2011 na uchaguzi mbili za rais mnamo 2014 na 2018 kuhudumu kama rais wa Uturuki.

Kuanzia mwaka 2002 hadi leo, chama chake kimeshinda kura tatu za maoni kuhusu mabadiliko ya katiba ambayo ni pamoja na kugeuza mfumo kutoka kwa kuwa wa kibunge hadi wa urais.

Chama cha Recep Tayyip Erdogan pia kilipata kura nyingi katika chaguzi zote za mitaa tangu 2002, idadi ambayo hakuna chama chochote cha kisiasa kiliweza kufikia tangu Uturuki kuhamia mfumo wa vyama vingi mwaka 1950.

Uchaguzi mkuu wa 2007

Baada ya uchaguzi wa rais wa 2007 kukwama kutokana na madai ya vitisho vya Kiislamu kwa urais na chama kikuu cha upinzani CHP kususia mchakato wa bunge wa kuchagua rais, Erdogan aliitisha uchaguzi mkuu wa mapema.

Chama cha AK kilishinda kwa wingi wa viti, 341 kati ya 550, kwa asilimia 46.58 ya kura.

Uchaguzi wa 2011

Uchaguzi wa mwaka 2011 ulileta ushindi wa tatu mfululizo kwa chama cha AK na rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan alichaguliwa tena kwa muhula wake wa tatu kama waziri mkuu. Chama cha AK kilipata asilimia 49.8 ya kura kikiwa na wabunge 327.

Uchaguzi wa rais wa 2014

Rais Recep Tayyip Erdogan alichaguliwa kuwa Rais wa 12 wa Uturuki kwa kura nyingi kabisa.

Ilikuwa mara ya kwanza, wananchi kushirikishwa katika uchaguzi wa rais kutokana na kura ya maoni ya katiba ya mwaka 2007 kuanzisha kura ya kitaifa ya moja kwa moja.

Uchaguzi mkuu na urais wa 2018

Muungano wa Wananchi, unaojumuisha Chama cha AK (asilimia 42.56) na MHP (asilimia 11.10) walipata asilimia 53.6 ya kura, ikiwa jumla ya viti 344 kati ya 600 katika bunge.

Siku hiyo hiyo ya uchaguzi mkuu, Rais Recep Tayyip Erdogan, mgombea wa Muungano wa Wananchi, alichaguliwa tena kuwa Rais wa 13 wa Jamhuri ya Uturuki, kwa asilimia 52.59 ya kura.

Rais Recep Tayyip Erdogan ameshinda kura tatu za maoni kuhusu mabadiliko ya katiba na kugeuza mfumo wa bunge la nchi kuwa kielelezo cha rais / Picha: AA

Kupungua kwa nguvu za kijeshi na jaribio la mapinduzi la 2016

Chini ya utawala wake, jukumu la uanzishwaji wa kijeshi wa Uturuki ndani ya mfumo wa kisiasa umepungua sana, na kuipa serikali ya kiraia mamlaka. Kabla ya utawala wa Recep Tayyip Erdogan, jeshi mnamo 1960, 1980 na 1997, iliondoa serikali kadhaa za kiraia zilizochaguliwa kidemokrasia. Uingiliaji kati ya kijeshi uliofanikiwa, unaoitwa mapinduzi ya baada ya kisasa, ulipindua serikali iliyoongozwa na Erbakan mnamo 1997.

Mnamo Julai 15, 2016, jaribio la mapinduzi lililoongozwa na kundi la waasi la jeshi lililochochewa na Fethullah Gulen, kiongozi wa Marekani wa Shirika la Kigaidi la Fethullah (FETO), lilishindwa kufuatia mwito wa rais wa Uturuki kwa raia wanaounga mkono demokrasia, kupigana na waliopanga mapinduzi mitaani.

Jaribio la mapinduzi liliua mamia ya raia na kujeruhi maelfu waliopigana kuyapinga. Kabla ya jaribio hilo la mapinduzi lililoshindwa, FETO ilikuwa imetumia njia zisizo halali kupenyeza taasisi za serikali ya Uturuki, kwa lengo la kuchukua udhibiti wa mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo.

Maendeleo kijeshi na viwanda vya Jeshi na Ulinzi wakati wa kazi ya kisiasa ya Rais Recep Tayyip Erdogan

Wakati wa urais wake, uwezo wa ulinzi wa taifa la Uturuki umeboreshwa kupitia ujumuishaji wa ubunifu wa kiteknolojia, ndege zisizo na rubani za Bayraktar Akinci zilizotengenezwa asilia zimekabidhiwa kwa Wanajeshi wa Uturuki.

Mafanikio ya ndege zisizo na rubani za Akinci yamejaribiwa katika migogoro ya Azabajani na Ukraine, na kuvutia tahadhari ya kimataifa. Sio tu katika mizozo ya kimataifa lakini pia katika operesheni dhidi ya shirika la kigaidi la PKK na YPG, kama vile "Operesheni Claw-Lock", imepatikana kuwa nzuri.

Ndege zisizo na rubani za Bayraktar zimejaribiwa katika mizozo mingi ya kimataifa kutoka Azerbaijan hadi Ukraine kupitia upatanishi wa serikali ya Uturuki, na kuibeba Uturuki katika nafasi muhimu katika siasa za dunia / Picha: AA

Pia, makombora ya kwanza ya anga hadi ardhini ya Uturuki, IHA-230, yaliyo tengenezwa na Baykar, yalifanyiwa majaribio kwa ufanisi tarehe 4 Aprili, 2023

Mbali na Bayraktar TB2s, na IHA-230, Hürjet imetengenezwa na kiwanda cha Turkish Aerospace Industries (TUSAŞ). Hürjet ni ndege ya kwanza ya kivita ya asili na ya kitaifa na ni ishara ya kujitolea kwa muda mrefu kwa ukuzaji wa viwanda na teknolojia ambazo zimeagizwa kutoka nje, kama Kamati Tendaji ya Sekta ya Ulinzi ilivyoeleza.

Uzinduzi wa TCG Anadolu

Kuundwa kwa sekta ya ulinzi endelevu imekuwa mojawapo ya malengo ya muda mrefu ya taifa la Uturuki wakati wa urais wa Recep Tayyip Erdogan. Meli ya kivita iliyojengwa ndani ya nchi TCG Anadolu, chombo cha kwanza duniani cha kubeba ndege ya kivita isiyo na rubani (UCAV), imewekwa katika jeshi la wanamaji la Uturuki tarehe 10 Aprili, 2023.

Kuboresha uwezo wa majini na kuongeza nguvu ya serikali ya Uturuki, ina uwezo wa kubeba helikopta, ndege zisizo na rubani, magari ya ardhini, na ndege za kivita.

Rais Recep Tayyip Erdogan aliboresha vituo vya majini vya jimbo la Uturuki na kuzindua TCG Anadolu kupitia maono yake ya kujitegemea Türkiye / Picha: AA

Kama Recep Tayyip Erdogan alivyosema, "TCG Anadolu...ni meli ya kwanza ya kivita duniani katika uwanja wake ambapo ndege spesheli zinaweza kutua na kupaa."

Mkakati wa Buluu: Kuhakikisha haki ya maji

Uwekezaji unaoongezeka katika vituo vya majini na vitendea kazi zaidi katika eneo la maji la Uturuki vimewakilishwa kupitia mkakati wa nchi wa ‘Blue Homeland’.

Mkakati huu wa ‘Blue Homeland’ umekumbatiwa na uongozi wa kisiasa wa Recep Tayyip Erdogan, ambao unaweka mkazo maalum juu ya ulinzi wa haki yake ya maji ya eneo na madai ya uhuru katika eneo lake la mamlaka ya baharini.

Kuongeza nguvu za majini, na maendeleo katika vifaa vya kuchimba visima imekuwa njia muhimu ya kutambua utimizaji wa mkakati wa sekta ya buluu ya nchi. Ilitetea uhuru kamili katika bahari ya mashariki ya Mediterrenean na Agean, ambayo inalenga kulinda haki za Waturuki wa Cypriots pia.

Uchimbaji katika maji ya eneo na usalama wa nishati

Madai ya uhuru yaliyopatikana kupitia mkakati wa ‘Blue Homeland’, yalisababisha kutumia uwezo wa njia za maji za Uturuki pia.

Ili kupunguza utegemezi wa nishati wa serikali ya Uturuki na kubadilisha vyanzo vya nishati, uwekezaji katika uchimbaji wa madini katika bahari ya Mediterrenean na bahari nyeusi, na katika mitambo ya nishati ya upepo na nishati ya nyuklia umeongezwa pia wakati wa uongozi wa kisiasa wa Erdogan.

Katika mchakato huu, Uturuki ilitumia njia zake za asili kuchimba visima na kuondoa hitaji la usaidizi wa makampuni ya kimataifa ya mafuta na uhandisi, kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa serikali ya Uturuki katika ujuzi wa uchimbaji wa nishati.

Uchimbaji wa kina katika hahari Nyeusi umetokana na ugunduzi mkubwa zaidi wa gesi asilia katika historia ya Uturuki, na kuipa Uturuki nafasi muhimu kiuchumi na kimkakati.

Uhuru wa nishati na usalama kwa kupunguza uagizaji wa nishati ni muhimu kwa maono ya enzi ya Erdogan, na ililenga kuifanya Uturuki kutokuwa na hali tete ya mabadiliko ya soko la kimataifa.

Hata hivyo, imekusudiwa pia kutumika kama nyenzo muhimu katika migogoro na mahusiano ya kimataifa ambayo huchangiwa na masuala yanayohusiana na usalama wa nishati.

Sekta ya ndani na kushindana kwa masoko ya kimataifa

Ili kuongeza uwezo wa tasnia ya kitaifa ya Uturuki na kuunganisha gari lenye chapa ya Kituruki katika masoko ya kimataifa kwa uchumi wa Uturuki wenye ushindani zaidi, gari la kwanza la umeme la Uturuki TOGG, limezinduliwa.

TOGG inalenga kuingia katika masoko ya kimataifa, kama Recep Tayyip Erdogan alisema, "Kufikia 2025, tutauza Togg duniani."

Gari la umeme ambalo ni rafiki kwa mazingira, TOGG, limeanzishwa wakati wa uongozi wa rais Recep Tayyip Erdogan / Picha: AA

Kupitia hii, inatarajiwa kwamba itapunguza nakisi ya biashara ya Uturuki kwa $ 7B, na kusababisha kuongeza fursa za ajira kwa raia, kama Recep Tayyip Erdogan alivyo elezea katika hafla ya uzinduzi wa TOGG.

Uturuki inayojitegemea na inayojitosheleza: Mafanikio ya sera za kigeni

Huku Recep Tayyip Erdogan ana wakosoaji ndani na nje ya Uturuki, uongozi wake ambao unalenga kuweka njia kwa Uturuki huru na inayojitosheleza, umemthibitisha kuwa ni hodari wa kubadilisha miungano na siasa Uturuki na kwingine ulimwenguni.

Taifa la Uturuki imekuwa na jukumu kubwa zaidi kupitia juhudi zake za kidiplomasia na msaada wa kijeshi katika mizozo ya kimataifa. Juhudi za Uturuki kuwa mchezaji wa kikanda zimejaribiwa kupitia mafanikio ya vifaa vyake vya kijeshi na uhusiano wa kidiplomasia ya kujaribu kusawazishwa na nguvu zingine.

Diplomasia kupitia miradi ya usalama wa nishati na bomba: TANAP na TurkStream

Chini ya uongozi wa Rais Erdogan Uturuki ilianzisha miradi ya bomba ambayo inaipa nafasi muhimu katika uhamishaji wa vyanzo vya nishati.

Bomba la Gesi Asilia la Trans-Anatolian (TANAP) linalobeba gesi ya Kiazabajani hadi Uturuki na Ulaya limefunguliwa mnamo 2018, likiimarisha jukumu la Uturuki kama kitovu cha nishati na kuwa hatua muhimu kwa usalama wa nishati.

TurkStream, iliyozinduliwa mnamo 2020, ni mradi mwingine, kuwezesha mtiririko wa nishati kutoka Urusi hadi Uturuki.

Ushirikiano katika tasnia ya ulinzi: Vita vya Armenia-Azerbaijan

Katika vita vya Armenia na Azabajani, utendakazi wa ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB2 zimevutia usikivu wa kimataifa, watunga sera na waangalizi wa tasnia na pia katika Syria, Iraqi Kaskazini na Libya zimeonekana kuwa za ufanisi na kupata uzoefu mkubwa wa serikali ya Uturuki.

Uturuki imekuwa mojawapo ya nchi sita zinazounda ndege zao zisizo na rubani na ilionyesha nia yake ya kushirikiana katika sekta ya ulinzi. Ushirikiano huo pia uliendelea baada ya vita, kwa kuzingatia zaidi misaada, ujenzi mpya na ujenzi wa miji ya Azerbaijan baada ya vita.

Jukumu la upatanishi: Vita vya Ukraine-Russia na Mkataba wa Nafaka

Mbali na mafanikio ya kijeshi yaliyothibitishwa katika maeneo yenye mizozo, Uturuki ilianza kutumia diplomasia laini kama mpatanishi.

Katika vita vya Ukraine na Urusi, Rais Recep Tayyip Erdogan alifanya mikutano kadhaa na mamlaka ya Ukraine na Urusi ili kumaliza vita.

Imekuwa kazi muhimu kwa serikali ya Uturuki kupatanisha Ukraine na Urusi kwa kuwa ndege zisizo na rubani zinazozalishwa na Uturuki zimetolewa kwa upande wa Ukraine dhidi ya malengo ya Urusi.

Mahusiano ya kusawazisha na pande mbili yalisaidia Uturuki kuhakikisha ushirikiano katika usalama na Ukraine upande mmoja na katika nishati, biashara na uchumi na Urusi kwa upande mwingine wakati wa msukosuko wa kiuchumi duniani.

Uturuki imekuwa mshikadau mkuu pamoja na Umoja wa mataifa katika majadiliano ya makubaliano ya nafaka na Urusi na Ukraine na baadaye kuongezwa kwa siku 120 kwa mpango huo.

Mkataba huo, ulioidhinishwa mwezi Julai mjini Istanbul, na Uturuki na Umoja wa Mataifa, ulihakikisha usafirishaji wa bidhaa za kilimo kutoka Ukraine, ambayo ni muhimu sana kwa usambazaji wa chakula duniani na kwa kuzuia uwezekano wa mgogoro wa chakula.

Kwa sababu hiyo, licha ya kubadili mwelekeo wa sera kadhaa za ndani na nje, uongozi wake umempatia wafuasi wengi ndani ya taasisi ya kisiasa ya Uturuki na miongoni mwa viongozi wengi wa kimataifa, kutoka Ukraine na Urusi hadi Afrika, Asia Pacific na Amerika ya Kusini. Pia katika majimbo ya Asia ya Kati na nchi zenye Waislamu wengi.

Katika uchaguzi wa Mei 14, Recep Tayyip Erdogan kwa mara nyingine tena analenga kushinda urais wake na mafanikio yake ya kisiasa, pamoja na wingi wa wabunge wa chama chake na chama cha People’s Alliance.

Wakati wa uongozi wake, Rais Recep Tayyip Erdogan alipata kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa, kutoka Ukraine na Urusi hadi Afrika, majimbo ya Asia ya Kati na nchi zenye Waislamu wengi/ Picha: AA
TRT World