Erdogan alipokea mamlaka yake kutoka kwa Spika wa Muda wa Bunge Kuu la Uturuki, Devlet Bahceli. / Picha: AA

Ikulu ya rais badae kidogo itakuwa mwenyeji wa sherehe ya kuapishwa, ambayo itahudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi 78, ikiwa ni pamoja na viongozi 21 wa nchi, mawaziri wakuu 13, na maafisa wa kiwango cha bunge na mawaziri.

Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na NATO, Shirika la Nchi za Kituruki (OTS), na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) pia watahudhuria.

Baada ya sherehe, Erdogan atakuwa mwenyeji wa chakula cha jioni katika Jumba la Cankaya, ambalo zamani lilikuwa nyumbani kwa marais wa Uturuki, baada ya sherehe saa 1:00 jioni saa za Uturuki.

Anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri baada ya chakula cha jioni.

Erdogan alishinda uchaguzi wa duru ya pili ya urais Jumapili iliyopita kwa kupata asilimia 52.18 ya kura.

Mgombea wa upinzani Kemal Kilicdaroglu alipata asilimia 47.82 ya kura, kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotolewa na Baraza Kuu la Uchaguzi la nchi.

TRT World