Erdogan pia "alielezea matumaini yake kwa muhula mpya kuwa wa manufaa kwa mahusiano ya Ututuki-Misri". / Picha:  AA

Nchi za Kiislamu zinapaswa kuendelea na juhudi zao za pamoja kwa ajili ya kusitishwa kwa mapigano ya kudumu katika Gaza, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemwambia mwenzake wa Misri Abdel Fattah el Sisi katika mazungumzo ya simu.

Wakati wa mazungumzo hayo siku ya Jumatano, viongozi hao wawili walijadili uchokozi wa Israel dhidi ya maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa, pamoja na juhudi za kutoa msaada wa kibinadamu kwa Gaza, kulingana na taarifa kutoka Idara ya Mawasiliano ya Uturuki.

"Katika maongezi yao, Rais Erdogan alisema ni muhimu kwa nchi za Kiislamu kuendelea na juhudi zilizoanzishwa ili kuhakikisha kusitishwa kwa mapigano ya kudumu kwa umoja," ilisema taarifa hiyo.

Pia ilibainisha kuwa rais wa Uturuki alimtakia Sisi, ambaye alichaguliwa tena kama rais wa Misri katika uchaguzi wa wiki iliyopita, heri njema.

Erdogan pia "alielezea matumaini yake kuwa muhula mpya utakuwa na manufaa kwa mahusiano kati ya Uturuki na Misri," iliongeza taarifa hiyo.

Israel imekuwa ikishambulia Ukanda wa Gaza tangu shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas, likiua angalau Wapalestina 19,667, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi wengine 52,586, kulingana na mamlaka za afya katika eneo hilo.

Mashambulizi ya Israel yameacha Gaza ikiwa magofu huku nusu ya makaazi ya eneo hilo la pwani yakiharibiwa au kuharibika, na karibu watu milioni 2 wakiwa wamehamishwa ndani ya eneo hilo lenye watu wengi wakikabiliwa na uhaba wa chakula na maji safi.

Inaaminika kuwa karibu Waisraeli 1,200 wameuawa katika shambulio la Hamas, huku zaidi ya mateka 130 wakiwa bado wanashikiliwa.

TRT World