Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameukaribisha uamuzi wa mataifa matatu ya Ulaya kutambua taifa la Palestina, akihimiza nchi nyingine kufanya maamuzi sawa na hayo.
"Nina furaha kubwa na matangazo ya leo" kutoka Norway, Ireland, na Hispania kwamba watatambua taifa la Palestina, alisema Erdogan wakati wa hotuba yake katika sherehe za Tuzo za Kimataifa za Ukarimu katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, siku ya Jumatano.
Uamuzi wa kutambua taifa la Palestina unakuja wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake mabaya Gaza, ambayo yamekuwa yakiendelea bila kikomo tangu Oktoba 7, 2023, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloitaka kusitisha mapigano mara moja.
“Wale wanaotoa msaada wa vifaa, kijeshi kwa wavamizi wanabeba jukumu sawa kwa damu inayoendelea kumwagika Gaza kama wavamizi wenyewe,” Erdogan aliongeza.
Alisisitiza kuwa mradi nguvu za Magharibi zitaendelea kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu licha ya “maji vuno na kutojali kwake,” mauaji katika Palestina hayawezi kuzuiliwa.
Gaza ni 'makaburi ya watoto'
Kiongozi wa Uturuki siku ya Jumatano alionya kwamba ikiwa upanuzi wa Kizayuni utaendelea hivi, dunia itakuwa “inakaribia kuanza migogoro mipya.”
"Israel imepoteza vita hii na imehukumiwa machoni pa ubinadamu," alisema, akisisitiza kwamba Tel Aviv imegeuza Gaza kuwa makaburi makubwa ya watoto katika siku 229 za mashambulizi.
Palestina tayari inatambuliwa na nchi nane za EU: Bulgaria, Poland, Czechia, Romania, Slovakia, Hungary, Sweden, na Kupro ya Kaskazini.
Zaidi ya Wapalestina 35,700 wameuawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na karibu wengine 80,000 wamejeruhiwa tangu Oktoba mwaka jana kufuatia shambulio lililofanywa na kundi la upinzani la Kipalestina la Hamas.
Zaidi ya miezi saba ya vita ya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yamebaki magofu katikati ya vikwazo vikali vya chakula, maji safi na dawa.
Israel inatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo imeamuru kuhakikisha vikosi vyake havifanyi vitendo vya mauaji ya kimbari na kuchukua hatua kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa kwa raia wa Gaza.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa amesema anatafuta hati za kukamatwa kwa viongozi wa Israel, akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kuhusiana na vitendo vyao wakati wa vita vya miezi saba vya Israel dhidi ya Gaza.