Uwezo wa ndege isiyokuwa na rubani ya Bayraktar TB3 wa kuruka kutoka umbali mfupi, unaashiria uimara wake katika masuala ya anga./Picha:AA  

Ndege isiyokuwa na rubani ya nchini Uturuki, Bayraktar TB3 imefanikiwa kufanya jaribio la kuruka kutoka kwenye meli ya kivita ya TCG Anadolu.

Chombo cha Bayraktar TB3, ambacho kimetengenezwa na kampuni ya ulinzi ya Baykar -ambayo ni kampuni kubwa nchini Uturuki-inakuwa ndege ya kwanza isiyokuwa na rubani katika historia ya anga, kuruka na kutua kutoka meli hiyo bila kutumia msaada wa vifaa vyovyote.

Baykar ni kampuni maarufu ya ulinzi ya nchini Uturuki iliyojikita katika utengenezaji wa ndege zisizo na rubani na teknolojia zingine za ulinzi.

Meli vita ya Uturuki iitwayo TCG Anadolu, ina uwezo wa kubeba helikopta, ndege nyuki, magari ya ardhini pamoja na vifaa vingine vya kivita.

Siku ya Novemba 19, ndege hiyo iliruka kutoka TCG Anadolu katika nyuzi 12, na kufanya jaribio la kuruka ka dakika 46 kwenye makutano ya bahari za Aegea na Mediteranea.

Tukio hilo linaashiria mafanikio makubwa katika teknolojia ya anga na ya majini.

Kampuni ya Baykar, imbayo inajulikana ulimwenguni kwa uwezo wa kuzalisha ndege zisizo na rubani, imedhirisha uwezo wa Uturuki katika kutengeneza vyombo hivyo.

Uwezo wa ndege isiyokuwa na rubani ya Bayraktar TB3 wa kuruka kutoka umbali mfupi, unaashiria uimara wake katika masuala ya anga.

Chombo cha TCG Anadolu kinatarajiwa kubeba vifaa viwili vya kutua, ndege na helikopta.

Ikiwa na urefu wa mita 231 na upana wa mita 32, chombo hicho kina uwezo wa kubeba uzito wa tani 27,000.

TRT Afrika