Ndege hii yenye ufanisi mkubwa ina uwezo wa kuruka angani ikiwa na uzito wa kilo 6,000/ Picha: AA  

Ndege isiyokuwa na rubani ya Bayraktar AKINCI, iliyotengenezwa na Baykar Technologies imefanikiwa katika jaribio lake la kurusha kombora la IHA-122 hivi karibuni.

Baykar, mhandisi wa ndege isiyo na rubani ya Uturuki, alishiriki kuelezea mafanikio hayo kwenye mtandao wa “X” na akatoa picha za jaribio la kufyatua makombora hayo.

Selcuk Bayraktar, afisa mkuu wa teknolojia wa Baykar, alishiriki picha ya jaribio la kurusha makombora kutoka AKINCI UCAV na kombora la IHA-122 kwenye akaunti yake ya “X”, iliyopewa jina la "Golden Age of Turkish Aviation."

Kupitia mtandao wa “X”, Murat Ikinci, mkurugenzi mkuu wa Roketsan, mtengenezaji wa makombora wa Kituruki, aliandika, "Tunajivunia kwa fahari katika njia hii tulioanzisha ya teknolojia yetu ya kitaifa."

Ikinci aliongeza, "Majaribio ya kombora la IHA-122 yamefanyika kwa ufanisi mkubwa sana. Nawapongeza wote waliohusika."

AKINCI ni ndege isiyo na rubani ya urefu wa juu, yenye kukaa angani kwa muda mrefu ikiwa na uzito wa kilogramu 6,000, ikilinganishwa na TB2 yenye kilo 700. Uzito wa Akinci wa kilogramu 1,500 ni mara 10 zaidi ya ule wa TB2.

TRT Afrika