Kituo cha kukabiliana na taarifa potofu kimegundua zaidi ya visa 250 ya kusambazwa kwa taarifa za uongo na Israeli kwa kutumia lugha sita./Picha:AA

Uturuki inapambana kukabiliana na taarifa potofu zinazosambazwa na Israeli kuhusu Palestina na vita vya Gaza, Mkurugenzi wa Mawasiliano nchini Uturuki, Fahrettin Altun amesema.

Kituo cha kukabiliana na taarifa potofu kimegundua zaidi ya visa 250 ya kusambazwa kwa taarifa za uongo kunakofanywa na Israeli kwa kutumia lugha sita ulimwenguni, alisema Altun wakati wa uzinduzi wa Jukwaa liliopewa jina la "Uongo wa Israeli" siku ya Jumatano.

"Wakati wa mkutano wa usalama mjini Munich, Rais wa Israeli Isaac Herzog aliinua kitabu akisema, ‘Jina la kitabu ni Mwisho wa Wayahudi, kilichopatikana na wanajeshi wetu huko Gaza. Kiliandikwa kwa na kiongozi mwandamizi wa Hamas Mahmoud al-Zahar.’ Hata hiyo, kitabu hichi kilichapishwa mwaka 1990 na mwandishi kutoka Misri asiye na mahusiano yoyote na Hamas wala Palestina.”

Katika hatua nyingine, Altun aligusia kuwa Israeli ilidai kuwa Hamas ilihusika na shambuliko kwenye hospitali ya al-Ahli Arab ya Gaza katika wilaya ya Zeitoun.

“Huu ulikuwa ni uongo mwingine tena,” alielezea. “Mashambulizi mfululizo ya Israeli dhidi ya hospitali huko Gaza yanadhihirisha kuwa Israeli inafanya hivyo bila kujali maadili ya kawaida ya kibinadamu.”

Upendeleo wa vyombo vya magharibi

Kulingana na Altun, lengo la Uturuki la kufichua yanayofanywa na Israeli kupitia jukwaa hilo, ni kutokueleweka kwa vyombo vya habari vya nchi za magharibi.

Alibainisha kuwa mwanzo wa vita hivyo, Israeli ilipokea msaada mkubwa wa kijeshi na wa kisiasa, pamoja na kuungwa mkono na vyombo vya habari ulimwenguni.

Hivi karibuni, Altun alidokeza kuwa hata jukwaa la kidijitali lilipiga marufuku filamu 19 zinazohusiana na Palestina, zikionesha sio tu kufutwa kabisa kwa uhuru wa kujieleza lakini pia uungwaji mkono wazi kwa moja ya "mauaji ya kikatili" zaidi katika historia.

Unafiki huu, kulingana na Altun, ni mfano wa wazi wa namna ubinadamu unayotolewa kafara kwa misingi ya kisiasa na kiuchumi, ili kufurahisha makundi ya Kisayuni.

Alieleza namna vyombo vya kimataifa vinavyopuuzilia mbali ghasia za Israeli huku akiwasilisha juhudi za kujilinda za Wapalestina kama vitendo vya chuki kwa hadhira ya kimataifa.

‘Kuuwawa’ au ‘kufa’

Tofauti ya lugha katika kuripoti habari inadhihirisha zaidi upendeleo huu, kwani matukio yanayohusisha Waisraeli yanaelezewa kama "kuuawa," huku visa kama hivyo vinavyowahusu Wapalestina zinalainishwa kuwa "walikufa", alisema.

Altun aliashiria mfano fulani ambapo chombo cha habari kinachoheshimika kimataifa kilirekebisha kichwa cha habari mara tatu kwa maslahi ya Israeli.

Hapo awali liliitwa "Shambulio la Israeli laua mamia hospitalini," kichwa cha habari kilibadilishwa kwa kuondoa "Israeli" na kisha kulainika zaidi kwa kubadilisha "shambulio" kuwa "mlipuko."

Nyingine ilisomeka , "Watu wapatao 500 waliuawa katika mlipuko wa hospitali huko Gaza," liliweka mkasa huo kama tukio la papo hapo, na kuficha dalili zozote za mhusika wa kweli, alisema.

Kulingana na Mkurugenzi wa Mawasiliano nchini Uturuki, Altun, mitindo hiyo ilifanya kazi kuuambia ulimwengu kuhusu upotoshaji huu wa ukweli.

‘Uongo wa Israeli’

Moja ya juhudi za Uturuki ni pamoja na jukwaa lililozinduliwa hivi karibuni, liliopewa jina la "Uongo wa Israeli", lenye malengo ya kukabiliana na taarifa potofu zinazoenezwa na Israeli na wafuasi wake.

Mkakati huo, uliozinduliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, unalenga kuweka kumbukumbu na kufichua simulizi za uongo zinazoenezwa na vyombo vya habari vya Israeli na kutoa ushahidi wa kweli katika lugha nyingi.

"Jukwaa letu linatumika kama ushuhuda wa uaminifu wa Uturuki kwa ajili ya ukweli na haki, kusimama kidete dhidi ya habari potofu na propaganda zinazozunguka mzozo wa Israeli na Palestina," alisema Altun.

Alielezea "Uongo wa Israeli" kama nyenzo muhimu ya kimataifa ambayo inalenga kujaza pengo kubwa katika mazingira ya vyombo vya habari duniani.

Jukwaa hilo hutambua na kupinga taarifa potofu za Israeli, na kusambaza maudhui yaliyothibitishwa kuhusu mzozo huo kwa hadhira ya kimataifa.

TRT Afrika