Kikundi cha ASALA hakikuilenga Uturuki tu, bali na nchi nyingine pia na kinakumbukwa kwa tukio la mlipuko wa bomu mwaka 1975 katika ofisi za Baraza la Makanisa ya Dunia mjini Beirut. / Picha: AA  

Erdogan Ozen, mwanadiplomasia wa Uturuki aliyeuwawa na kikundi cha kigaidi cha Armenia mwaka 1984, amekumbukwa kwenye mji mkuu wa Austria.

Shughuli ndogo iliandaliwa nje ya ubalozi wa Uturuki siku ya Alhamisi kama ishara ya kumkumbuka naibu balozi huyo, miaka 40 baada ya kuuwawa na kikundi cha kigaidi cha Armenia cha ARA, Juni 20 mjini Vienna.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Balozi wa Uturuki nchini Austria Ozan Ceyhun alikumbusha kuwa wanadiplomasia wa Uturuki walilengwa na makundi ya kigaidi ya Armenia kwenye miaka ya 70 na 80.

Walitafutwa kwa kuwa tu walikuwa ni Waturuki, wakiwakilisha Uturuki, aliongeza Ceyhun.

Akidokeza kuwa askari wa Austria pia aliuwawa katika shambulio hilo, balozi huyo wa Uturuki alikumbuka namna ambavyo jumla ya watu 77, kati yao hao, 58 wakiwa ni raia wa Uturuki, wakiwemo wanadiplomasia 31 na ndugu zao, walivyopoteza maisha katika mashambulizi ya kutoka 1973 hadi 1986.

Levent Eler, Mwakilishi wa Kudumu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna, Hatun Demirer, Mwakilishi wa Kudumu kutoka Uturuki katika Shirika la Ushirikiano wa Usalama la Ulaya (OSCE) na mke wa mwanadiplomasia huyo Monika Ozer, walihudhuria kumbukumbu hiyo.

Mashambulizi hayo yalianza mwaka 1973 wakati Balozi wa Uturuki mjini Los Angeles Mehmet Baydar na mwanadiplomasia Bahadir Demir walipouwawa na kikundi cha kigaidi kiitwacho Gourgen Yanikian.

ASALA kilikuwa ni kikundi cha kwanza cha kigaidi kutoka Armenia kuanza kuishambulia Uturuki.

Mashambulizi yao hayakuwalenga Waturuki tu, bali na nchi nyingine pia na kinakumbukwa kwa tukio la mlipuko wa bomu wa mwaka 1975 katika ofisi za Baraza la Makanisa ya Dunia mjini Beirut.

TRT Afrika