Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye mkutano wa 29 wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ulimwenguni (COP29).
Erdogan alifanya mazungumzo hayo na Erdogan katika nafasi yake kama mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Watu Mashuhuri wanaoshughulikia utokomezaji wa taka kwenye mkutano huo wa COP29.
Kikao hicho kiliangazia juhudi za mradi wa kutokomeza taka, ulioasisiwa chini ya udhamini wa Emine Erdogan, pamoja na masuala mengine yenye kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na uhifadhi wa mazingira.
Wakati wa mkutano huo, Erdogan alimshirikisha Guterres kuhusu juhudi zinazoendelea dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi zinazofanywa na Bodi ya Ushauri ya Watu Mashuhuri wanaoshughulikia utokomezaji wa taka, ambayo yeye ndiye mwenyekiti.
Mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi
Uturuki imejiweka kwenya nafasi kama kinara wa mazingira endelevu ulimwenguni, huku mke wa Rais Emine Erdogan akiwa mstari wa mbele kwenye jitihada za taifa lake.
Tangu achukue wadhifa wake kama mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Mataifa utokomezaji taka , Mke wa Rais Emine Erdogan amekuwa na jukumu muhimu katika kuendeleza Mradi kabambe wa Uturuki kusukuma mbele azma hiyo.
Ilizinduliwa chini ya udhamini wake mnamo 2017, mpango ambao unalenga kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupunguza taka kwenye chanzo chake, kuboresha matumizi ya rasilimali, na kukuza juhudi za kuzirejeza nchini kote.