Ujasusi wa Uturuki ulmkata makali  msafirishaji wa Irak-Syria,  aliyewezesha harakati za magaidi na silaha kote Gara, Zap, Metina, na Haftanin, katika operesheni iliyofanywa huko Gara. /Picha: AA

Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) "limemkata makali " gaidi mkuu wa PKK Kaskazini mwa Iraqi, upande wa pili wa mpaka wa Uturuki, vyanzo vya usalama vilisema.

Kadri Encu, aliyepewa jina la Dogan, alikatwa makali katika mkoa wa Gara wa Iraq, vilisema vyanzo vya habari Jumapili, ambavyo vilizungumza kwa sharti la kutokujulikana kwa sababu ya vizuizi vya kuzungumza na vyombo vya habari.

Encu, alikuwa akitoa njia kwa makundi ya kigaidi katika maeneo ya kaskazini mwa Iraq ya Gara, Zap, Metina na Haftanin, kufanya mashambulizi dhidi ya eneo la Operesheni ya kupambana na ugaidi ya Uturuki, iliongeza.

Kulingana na vyanzo, Encu alikuwa afisa anayejulikana kama afisa wa Iraq-Syria wa magaidi wa PKK, alijiunga na safu ya vijijini ya kikundi hicho mnamo 2006, na akapewa mafunzo katika mkoa wa Zap.

Alifanya kama mlinzi wa Duran Kalkan, aliyepewa jina Abbas, na alikuwa mwanachama wa kile kinachoitwa baraza kuu la PKK mnamo 2015-2017. Alienda Gara kama afisa wa usafirishaji wa Iraq-Syria mnamo Januari 2018, vyanzo viliongeza.

Mbali na kile kinachojulikana kama majukumu ya mjumbe, duru hizo zilisema, Encu pia alihusika katika shughuli za kitengo cha uhusiano wa kigeni cha kikundi cha kigaidi na alipanga uhamishaji wa magaidi na silaha za PKK ndani ya Iraq na kati ya Iraq na Syria.

Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "kukatwa makali " kumaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha nje ya mpaka, kaskazini mwa Iraq, kupanga mashambulizi.

Uturuki ilizindua Operesheni Claw-Lock mwaka jana mwezi Aprili ili kulenga maficho ya kundi la kigaidi la PKK katika mikoa ya Metina, Zap, na Avasin-Basyan kaskazini mwa Iraq, iliyoko karibu na mpaka wa Uturuki.

Ilitanguliwa na operesheni mbili - Claw-Tiger na Claw-Eagle - zilizoanzishwa mnamo 2020 kuwaondoa magaidi waliojificha kaskazini mwa Iraqi na kupanga njama za kuvuka mpaka huko Uturuki.

Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki , PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU - imehusika na vifo vya karibu watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, na watoto.

TRT World