Mafuriko makubwa yanayosababishwa na El Nino yamesababisha uharibifu nchini Somalia. / Picha: AA Archive

Somalia imepokea raundi ya pili ya misaada ya kibinadamu kutoka Uturuki, iliyowalenga wale walioathiriwa na mafuriko makubwa ya hivi karibuni nchini humo yaliyotokana na El Nino.

"Msaada huu unakusudiwa kusambazwa kwa waathiriwa wanaokabiliwa na shida kote nchini," Kamishna wa shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga Somalia Mahamuud Moallim, ambaye alipokea msaada huo, alisema, akitoa shukrani kwa Uturuki kwa msaada wake katika wakati huu mgumu.

Msaada huo ni wa pili kutoka Turkish Red Crescent kufika katika taifa hilo la Pembe ya Afrika tangu misaada ya mafuriko ilipoanza katikati ya Oktoba mwaka huu.

Mafuriko makubwa yaliyosababishwa na matukio El Nino, ambayo yalitangazwa kuwa "hali ya dharura ya kitaifa" na serikali ya Somalia mnamo mwezi uliopita, yameua zaidi ya watu 100, yakiwahamisha zaidi ya 750,000, na kwa ujumla yameathiri zaidi ya wakazi milioni 2 nchini humo.

Vifaa vya Vyombo vya Habari vya Gambia

Mnamo Jumanne, Shirika la ushirikiano na Uratibu la Uturuki (TIKA) lilitoa vifaa vya vyombo vya habari vya kiufundi kwa Gambia, nchi ya Afrika Magharibi ambayo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka ujao wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Shirika hilo la misaada liliipa Idara ya Redio na Televisheni ya Gambia (GRTS), taasisi ya zamani na kuu ya utangazaji wa umma nchini, na vifaa vya kizazi kipya, TIKA ilisema katika taarifa.

Sherehe ya utoaji ilifanyika katika mkoa wa Serekunda na ushiriki wa Balozi wa Uturuki nchini Gambia Tolga Bermek, mratibu wa ofisi ya Tika Banjul Sule Bayar, maafisa wa Wizara ya Habari, wafanyikazi wa GRTS, na waandishi wa habari.

Waziri wa Habari wa Gambia Lamin Jammeh alisema msaada wa TIKA ulikuwa muhimu katika kuongeza miundombinu ya kiufundi na uwezo wa matangazo ya moja kwa moja ya GRTS. Aliwashukuru TIKA na Uturuki kwa michango yao muhimu.

AA