Ndege mbali mbali za kisasa zilikuwepo kwenye maonesho hayo./Picha: TRT Afrika

Na Susan Mwongeli

TRT Afrika, Adana, Uturuki

Maaonesho makubwa zaidi ya teknolojia ya anga nchini Uturuki, maarufu kama Teknofest, yameshika kasi huko Adana, jiji la kusini nchini humo. displays.

Maonesho hayo ya siku tano, yalianza siku ya Jumatano huku kukiwa na shamrashamra na shauku kubwa kutoka kwa watazamaji mbalimbali.

Tukio hilo lilitawaliwa na maonesho ya ndege za jet, ndege vita, ndege zisizokuwa na rubani, helikopta na maonesho mengine.

Mbali ya vifaa vya angani onesho hilo pia lilihusisha teknolojia zingine kama vile ndege nyuki yaani 'drone' za chini ya maji.

‘’Teknolojia ni kitu muhimu sana ulimwenguni, kama inavyojidhihirisha hapa Adana nchini Uturuki,’’ Yavuz Selim Köşger, gavana wa mji wa Adana anaiambia TRT Afrika.

‘’Maonesho haya yanadhihirisha hatua ya Uturuki kwenye nyanja ya teknolojia ya ulinzi. Tunahitaji vijana wadogo kuelewa uwezo wa nchi yetu,’’ alisisitiza.

Maonesho hayo ya siku tano, yalianza siku ya Jumatano huku kukiwa na shamrashamra na shauku kubwa kutoka kwa watazamaji mbalimbali./Picha: TRT Afrika

Onesho hilo lililoandaliwa kwa pamoja, kati ya Taasisi ya Teknolojia ya Uturuki (T3) na Wizara ya Viwanda na Teknolojia toka mwaka 2018, kwa kushirikiana na wizara mbalimbali, vyuo vikuu na taasisi za umma.

Wahudhuriaji wa maonesho hayo hupata fursa ya kushuhudia teknolojia mbalimbali za hali ya juu, sambamba bunifu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani.

‘’Leo nimekuja kwa ziara ya masomo kuja kuona mambo mazuri yanayofanywa na nchi yanayofanywa na nchi yangu. Nimeona ndege na vitu mbalimbali, najisikia fahari na nchi yangu. Imeamsha ari kubwa sana ndani yangu ya kuelezea mawazo niliyonayo na kufanya vitu kama hivi,’’ mwanafunzi mmoja anayehudhuria maonesho hayo aliiambia TRT Afrika.

Katika siku ya kwanza ya maonesho hayo makubwa ya teknolojia, ndege isiyokuwa na rubani iliyotengenezwa na Baykar, iitwayo TB3 iliruka kwa mara ya kwanza..

Chombo hicho kiliruka angani sambamba na Bayraktar Akinci, ndege nyingine isiyokuwa na rubani wakati wa maonesho hayo, yaliyofanyika Adana.

Pia, kulikuwa na maonesho ya ndege nyuki na maroboti.

Onesho hilo lililoandaliwa kwa pamoja, kati ya Taasisi ya Teknolojia ya Uturuki (T3) na Wizara ya Viwanda na Teknolojia toka mwaka 2018, kwa kushirikiana na wizara mbalimbali, vyuo vikuu na taasisi za umma./Picha: TRT Afrika

Onesho hilo lilihusisha maonesho mbalimbali ya kuvutia, na magari mbalimbali ya ardhini, yaliyomwacha kila mtu kinywa wazi.

Toka kuanzishwa kwake mwaka 2018, onesho hilo limezidi kukua, siku hadi siku, likivutia watu wengi kila mwaka.

Kinachovutia zaidi ni kwamba, onesho hilo halifanyiki sehemu moja maalumu. Huandaliwa katika maeneo tofauti nchini Uturuki, na hata liliwahi kufanyika nchini Azerbaijan miaka miwili iliyopita.

Wakari wa kusherehekea miaka 100 ya Jamhuri ya Uturuki, onesho la Teknofest lilifanyika katika miji ya Ankara na Izmir.

Maonesho hayo ni makala ya 10 ya Teknofest.

TRT Afrika