Ndege ya kukodi iliyokuwa imebeba raia wa Uturuki 169, imewasili katika uwanja wa ndege wa Istanbul, ikitokea Lebanon.
Ndege hiyo iliwasili siku ya Alhamisi, baada ya kusimama katika uwanja wa ndege wa Cukurova ulioko Adana, kusini wa Uturuki, ambapo abiria 110 walishuka.
Baadhi ya abiria walishindwa kuficha hisia zao za furaha mara baada ya kufika nchini Uturuki.
Watu hao waliondoka kwenye eneo la uwanja wa ndege mara baada ya shughuli za ukaguzi wa hati za kusafiria kukusanya mizigo yao.
Uturuki iliandaa mpango huo wa kuwaondoa raia wake kwa kutumia ndege hiyo ya kukodi, ambayo iliondoka Beirut asubuhi ya tatu, kama hatua muhimu ya kuwalinda raia wake katikati ya mashambulizi ya Israeli.
Hapo awali, Meli za Kivita za Uturuki ziliokoa takribani watu 1,000 kutoka eneo la Lebanon, wakiwemo raia wa Uturuki 878 na wengine 24 kutoka sehemu ya kaskazini mwa Cyprus.
Israeli imekuwa ikiendesha mashambulizi mfululizi dhidi ya Lebanon kuanzia Septemba 23 dhidi ya kile wanachokiita Hezbollah, huku wakiua zaidi ya watu 1,500 na kujeruhi wengine zaidi ya 4,500.