Maelfu ya waandamanaji wakitembea Istanbul kuiunga mkono Palestina siku ya kwanza ya mwaka mpya huku Israeli ikiendelea na mauaji ya halaiki Gaza. Picha: AA

Mamia na maelfu ya watu wametembea Istanbul, wakishiriki tukio kubwa lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana Uturuki (TUGVA) chini ya kauli mbiu, "Amsha Dunia."

Mapema kuanza kwa mwaka mpya, watu wakiwa na mabango yanayosema 'Mwisho wetu ni Daraja la Galata,' walianza kukusanyika baada ya swala wa alfajiri katika Msikiti Mkubwa wa Aya Sofya kuonyesha mshikamano wao na Palestina.

Makumi kwa maelfu waandamana Istanbul kuiunga mkono Palestina katika siku ya kwanza ya mwaka mpya huku Israeli ikiendelea na mauaji ya halaiki Gaza. Picha: AA

Waandamanaji wengi walivaa vitambaa vya 'keffiyeh' kuonyesha kuiunga mkono Gaza na walibeba mabango yakiwa na maandishi kama vile "Jerusalem ni yetu," "Gaza: Ambapo Watoto Hawakui," na "Jerusalem imekaliwa."

Wengine waliwasha tochi wakati wakitembea, mara kwa mara wakiimba kwa kusema "Muuaji Israeli atawajibishwa," "Mashuhuda daima hawafi," na "Kutoka Istanbul mpaka Al-Aqsa, salamu elfu moja kwa wanaopambana."

Baada ya kufika Daraja la Galata, washiriki walikaguliwa na polisi kabla ya kuingia eneo la tukio.

Makumi kwa maelfu waandamana Istanbul kuiunga mkono Palestina katika siku ya kwanza ya mwaka mpya huku Israeli ikiendelea na mauaji ya halaiki Gaza. Picha: AA

Mashirika ya misaada yalijitolea chai, mikate ya simit, na supu kwa waliohudhuria, huku mamlaka ikihakikisha kuna usalama wa hali ya juu katika eneo la msikiti na daraja.

Mkusanyiko huu unatilia msisitizo mafungamano ya kihistoria na kitamaduni yaliyopo kati ya Uturuki kwa Jerusalem na Al-Aqsa, huku washiriki wakitaka dunia kwa ujumla kuchukua hatua na kuunga mkono harakati za Palestina.

TRT World