Wajumbe wa bodi ya uchaguzi wa Ng'ambo wanaanza kuainisha kura zilizopigwa nje ya nchi na wananchi wa Uturuki  katika Ukumbi wa ATO Congresium jijini Ankara, Uturuki mnamo Mei 12, 2023

Kinyume na mashaka ambayo baadhi ya mashirika ya habari ya kimataifa yameibua katika siku za hivi majuzi, mchakato wa kupiga kura na kuhesabu unaofuata umeundwa kwa njia ya kupunguza uwezekano wa kuibiwa.

Zaidi ya watu milioni 60 wanastahili kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge wa Mei 14 ambao unafanyika katika majimbo 81 chini ikitazamiwa kwa ukaribu na vyombo vya habari. Zoezi hilo linahusisha kufuatilia masanduku 191,000 ya kura. Na kutakuwa na macho yakiangalia zoezi hili.

Watu walio nje ya nchi kupiga kura

Karibu Waturuki milioni 6.5 wanaishi katika nchi zingine. Miongoni mwao, milioni 3.28 walistahili kupiga kura katika uchaguzi huu wa urais na ubunge.

Ikilinganishwa na wapiga kura milioni 60.9 waliojiandikisha ndani ya Uturuki, kura za walioishi nje ya nchi zinaweza kuonekana kuwa ndogo, na serikali ilichukua kila hatua zinazo hitajika ili kuhakikisha usalama wa masanduku ya kura kwenye mipaka katika nchi ambazo waturuki wanapiga kura zao.

Kufuatia kukamilika kwa upigaji kura, mifuko iliyotiwa muhuri hutumwa Uturuki ikisindikizwa na wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo, na kufungiwa ndani ya chumba hadi upigaji kura uishe Uturuki na kuhesabu kura kuanza.

Wengi wa watu wanaoishi nje ya Uturuki wanaishi Ulaya Magharibi, ambapo wafanyakazi wahamiaji waliishi katika miaka ya 1960 kama sehemu ya mpango wa ujenzi wa baada ya vita vya dunia vya pili. Wanaunda kundi moja kubwa zaidi la wahamiaji Waislamu Ulaya Magharibi.

Ikiwa na zaidi ya wapiga kura milioni 1.5 waliojiandikisha kutoka nje ya nchi, Ujerumani inaongoza katika orodha ya nchi ambazo siasa za Uturuki zitaonekana sana kuwa katika hali ya joto, ikifuatwa na Ufaransa, Uholanzi na Ubelgiji.

Baraza kuu la uchaguzi Uturuki (YSK) limeweka mfumo ambao unahakikisha uadilifu wa kura kuanzia kwenye vituo vya kupigia kura.

Katika kila kituo cha kupigia kura, bodi ya wanachama watano, ambayo inajumuisha wawakilishi wa YSK na vyama vikuu vya kisiasa, imeteuliwa.

Bodi hukagua utambulisho wa wapiga kura na ikiwa majina yao yamejumuishwa katika orodha ya wapiga kura.

Hii inaondoa uwezekano wa mtu mmoja kupiga kura mara mbili. Pia husaidia kujenga maelewano kati ya pande husika juu ya matokeo.

Vyama vya kisiasa vikiwemo Chama cha AK na upinzani CHP, ambacho ni sehemu ya Muungano wa vyama sita vya Nation Alliance, vitatuma makumi ya maelfu ya waangalizi kwenye vituo vya kupigia kura.

Uchaguzi katika mikoa iliyokumbwa na tetemeko

YSK pia imefanya mipango maalum ya kuwezesha wapiga kura katika majimbo 11 yaliyokumbwa na matetemeko mabaya ya ardhi ya tarehe 6 Februari.

Takriban watu 300,000, ambao wana haki ya kupiga kura, na wamehamia miji mingine baada ya maafa wamejiandikisha katika mfumo maalum wa kupiga kura bila kuhitaji kusafiri kurudi katika miji yao.

Katika wiki chache zilizopita, wajumbe kadhaa wa YSK walitembelea eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi ili kutathmini hali na kupata kile kinachohitajika kuendesha uchaguzi.

Maelfu ya waangalizi watafuata uchaguzi

Kabla ya uchaguzi, vyama vinaajiri maelfu ya watu wa kujitolea hasa kwa madhumuni haya. Wawakilishi hawa wana ruhusa ya kuandamana na masanduku ya kura.

Kando na wawakilishi wa vyama na maafisa wa YSK, mashirika yasiyo ya serikali yana watu wao wa kujitolea kufuatilia upigaji kura.

Shirika lisilo la serikali linaloitwa moja, ‘Vote and Beyond’, linasema limetenga takriban watu 100, 000 kukusanya matokeo ya kupiga kura.

Watu wa kujitolea wa vyama vya siasa watakuwepo vituoni kuisimamia shughuli ya kuhesabu kura inapoanza.

Wataweza kujumlisha kura, kupiga picha na kusambaza taarifa hizo kwa wakuu wa vyama.

Kinachofanya mchakato wa uchaguzi kuwa wa uwazi zaidi ni uwepo wa waangalizi huru ikiwa ni pamoja na timu ya wajumbe 40 wa Baraza la Ulaya na Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) ambao wamekuja kwa mwaliko wa serikali.

Uhuru wa bodi kuu ya uchaguzi ulidhihirika mapema mwezi huu ilipokataa ombi la serikali la kutoa taarifa ya maeneo ambapo masanduku ya kura yatakuwa kabla ya uchaguzi.

Upinzani haukuunga mkono swala hili la kutaka bodi ya uchaguzi kutoa taarifa hii kwa wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki.

Hii inaendelea tu kuonyesha kwamba halmashauri za kusimamia uchaguzi zinafanya kazi bila kutegemea siasa na ushawishi wa serikali.

Ili kuepuka mkanganyiko wowote, ni Shirika rasmi la serikali la Anadolu pekee ndilo lililoidhinishwa kutoa matokeo ya uchaguzi.

TRT World