Gwaride hilo maalumu lenye kulenga kuimarisha umoja na mshikamano na kukuza uhusiano wa kiuchumi na kiutamaduni kati ya jumuiya ya Waturuki na Wamarekani, litafanyika jijini New York, kuanzia Mei 17 hadi 18.
Gwaride la Siku ya Uturuki, ambalo linalenga kuonesha mshikamano dhidi ya mauaji ya wanadiplomasia wa Uturuki na shirika la kigaidi la Armenia ASALA nchini Marekani, liliandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1981 na tangu wakati huo limekuwa tukio la kitamaduni.
Chini ya uratibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, gwaride hilo litafaanza kwa kupandishwa kwa bendera ya katika bustani ya umma ya Bowling Green, Mei 17.
Kama sehemu ya shamrashamra hizo, Mei 17, jopo lililopewa jina la "Kuimarisha Mahusiano ya Kitamaduni: Dira Mpya ya Uhusiano wa Uturuki na Marekani" litaandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais katika Ikulu ya Uturuki.
Jopo hilo linalowashirikisha wasomi wa Uturuki na Marekani na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, litaangazia masuala ya kitamaduni ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Zaidi ya hayo, hali ya sasa ya mahusiano ya Uturuki na Marekani na mustakabali wa mahusiano haya katika muktadha wa kitamaduni utatathminiwa.
Zaidi ya hayo, maonesho maalumu, ya "Karne ya Uturuki" yatafanyika katika Jumba la Uturuki. Kupitia maonyesho maalum ya kidijitali, maonyesho hayo yataonyesha mafanikio ya Uturuki katika kipindi cha miaka 100 iliyopita katika muundo wa pande tatu.
Michezo maalum na shughuli za burudani pia zitaandaliwa kwa ajili ya watoto.