Zoezi la kurudisha miili hiyo limefanyika kusini mwa Gaza katika mji wa Khan Younis. / Picha: AFP

Hamas imekabidhi kwa Shirika la Msalaba Mwekundu miili ya mateka wanne waliouliwa katika mashambulizi ya Israeli Gaza, kwa mujibu wa TRT World.

Shirika la Msalaba Mwekundu limeelekea sehemu ya Gaza kupokea miili ya mateka wanne wa Israeli ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya usitishaji wa mapigano, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israeli.

Zoezi la kupeana kwa miili hiyo limefanyika kusini mwa Gaza katika mji wa Khan Younis.

Kabla ya kuwasilishwa kwa miili hiyo, mamia ya watu walikusanyika katika eneo lililotumika kama makaburi. Kumewekwa uzio ili kuzuia watu kufika katika eneo lililotengwa kufanyika zoezi la kupeana miili hiyo.

Hamas imeonyesha majeneza manne yaliyowekwa katika jukwaa Gaza.

Hamas imesema itapeana miili ya Shiri Bibas, Kfir, Ariel, na Oded Lifshitz.

TRT World