Fidan: Kikundi maalumu cha Gaza kinafanya kila jitihada kuzuia mauaji ya kimbari ya Israeli

Fidan: Kikundi maalumu cha Gaza kinafanya kila jitihada kuzuia mauaji ya kimbari ya Israeli

Hakan Fidan ahudhuria kikao cha Taasisi ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) and Umoja wa nchi za kiarabu uliofanyika jijini New York.
Kikundi hicho kimehusika kikamilifu katika michakato ya kidiplomasia ya kutafuta suluhu ya vita vya Israeli katika eneo la Gaza./ Picha: AA  

Kikundi maalumu cha Gaza kimefanya kila liwezekanalo kuzuia mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israeli katika eneo la Gaza, Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan amesema.

Fidan alihudhuria kikao cha Taasisi ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) and Umoja wa nchi za kiarabu uliofanyika jijini New York, siku ya Jumapili, kando ya kikao cha 79 cha Baraza la Umoja wa Mataifa (UNGA), kilichofanyika jijini New York.

Kundi hicho kimekuwa "kikifanya kila liwezekanalo" kuongeza ufahamu wa kimataifa kuhusu mashambulizi yanayoendelea dhidi ya raia wa Palestina, Fidan aliuambia mkutano huo.

"Wiki hii, wakati wa mikutano yetu na majadiliano ya pande mbili, lazima tuzingatie hali mbaya nchini Palestina ," alinukuliwa akisema.

Kundi hilo, ambalo lililoundwa katika Mkutano wa Kilele wa Umoja wa OIC na Umoja wa Nchi za Kiarabu huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, Novemba mwaka jana, limekuwa likijihusisha kikamilifu katika mipango ya kidiplomasia katika miji mikuu mbalimbali ya kimataifa kutafuta suluhu kuhusu vita vinavyoendelea vya Israeli huko Gaza.

TRT Afrika