"Zile siku ambazo siasa ilifungamana na ugaidi zimeisha," amesema Erdogan ./ Picha: AA  

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitizia mabadiliko chanya yanaonekana katika majimbo ya mashariki na kusini mashariki mwa Uturuki, baada ya kukombolewa kutoka kwenye ugaidi, kufuatia juhudi za serikali.

"Kadiri vivuli vyeusi vya kigaidi vinavyozidi kupotea katika majimbo hayo, ndivyo uwezo wa maeneo hayo unavyojidhihirisha ," alisema Erdogan siku ya Jumamosi, wakati akihutubia ufunguzi wa vituo vya uwekezaji vya Bitlis .

Alisisitiza faida zinazoonekana za mabadiliko haya, akisema: "Ni jana tu, eneo la Mlima Gabar lilikuwa ni kitovu cha ugaidi; leo hii, eneo hilo limekuwa ndio chanzo kikubwa cha hifadhi ya mafuta nchini.

"Zile siku ambazo siasa ilifungamana na ugaidi zimeisha,"aliongeza.

Matamshi ya Erdogan yanaonyesha mwelekeo mpana wa uzindukaji wa maeneo ambayo hapo awali yalikumbwa na migogoro, ambayo kwa sasa yanashuhudia maendeleo makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo kadri usalama unavyoimarika.

TRT Afrika