Uturuki, ambayo ni mshirika wa NATO imekosoa mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza na kile inachokiita msaada inaoupata kutoka nchi za Magharibi./Picha: AP  

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan ameingia kwenye mjadala kuhusu maandamano ya ya vyuo vikuu nchini Marekani, akisema mamlaka zinaonyesha "ukatili" kwa kuwakandamiza wanafunzi na wasomi wanaoiunga mkono Palestina.

"Wanafunzi makini na wasomi wakiwemo Wayahudi wanaopinga Uzayuni kwenye baadhi ya vyuo vikuu vikubwa vya Marekani wanapinga mauaji hayo (huko Gaza)," alisema Erdogan wakati akiwa Ankara.

"Watu hawa wanafanyiwa vurugu, na kupitia ukatili na mateso makubwa kwa kuwa tu wanapinga mauaji ya Israel na kutaka yakomeshwe," alisema na kuongeza kuwa wafanyakazi wa chuo kikuu "wanafukuzwa kazi na kuuawa" kwa kuwaunga mkono Wapalestina.

"Mipaka ya demokrasia ya Magharibi iko kwa maslahi ya Israeli," Erdogan alisema. "Chochote kinachokiuka maslahi ya Israeli ni kinyume na demokrasia, kinyume na imani kwao."

TRT Afrika