| Swahili
UTURUKI
1 DK KUSOMA
Erdogan ahudhuria kikao cha kukabiliana na njaa kwenye mkutano wa G20
Mkutano Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20 unafanyika katika jiji la Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Erdogan ahudhuria kikao cha kukabiliana na njaa kwenye mkutano wa G20
Rais wa Uturuki Erdogan akiwa na mwenzake wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov, ambao walipata muda wa kuteta./Picha: AA   / Others
18 Novemba 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amehudhuria kikao cha Ushirikishwaji wa Kijamii na Mapambano dhidi ya Njaa na Umasikini wakati wa Mkutano Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20, unaofanyika nchini Brazil.

Mkutano huo unafanyika kwenye jumba la makumbusho jijini Rio de Janeiro.

Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, makala maalumu ya kuhusu baa la njaa ilioneshwa.

Rais Erdogan alikaa karibu na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov, wakati wa kikao hicho, na wakapata wasaa wa kuteta.

Kikao hicho kiliendelea baada ya hotuba ya Rais wa Brazil Lula da Silva.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika