Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan./Picha: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amehakikishia utayari wa Uturuki kulinda umoja wa Syria na kuwaunga watu wake, akionya dhidi ya majaribio ya kuivuruga nchi hiyo.

Akizungumzia mustakabali wa Syria, Erdogan alisisitiza msimamo wa Uturuki dhidi ya mgawanyo na mgogoro katika kanda hiyo.

“Hatuwezi kuruhusu Syria igawanyike tena,” alisema Erdogan.

“Shambulio lolote dhidi ya uhuru wa watu wa Syria na utulivu wa utawala wake mpya utatufanya tusimame upande wao,” aliongeza.

Kupinga uchokozi

Erdogan alionesha wasiwasi kuhusu vitendo vya kichokozi vinavyolenga kuwazuia raia wa Syria kurudi kwao.

“Tunapinga kila aina ya vitendo au uchokozi vitakavyosababisha ndugu zetu wa Syria kurejea kwao,” alisema , huku akisisitizia utayari wa Uturuki kudumisha amani ya kanda.

Pia alionya dhidi ya hila za kiitikidi na kijiografia zenye kuhatarisha usalama wa kanda.

“Hatutosimama kizembe huku watu fulani waliolewa madaraka wakiendelea kuitumbukiza kanda yetu katika damu na moto,” alisema.

Kukanyaga makundi ya kigaidi

Akisema kuwa nchi yake itaendelea kusimama na Wasyria walioko Uturuki ambao wako njiani kurejea Syria, Erdogan aliongeza kuwa vikundi vya kigaidi vya Daesh na PKK/PYD vilivyoko Syria vitamalizwa siku si nyingi.

Jeshi la Israeli lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Syria kufuatia kuanguka kwa utawala wa Bashar al Assad, kituo cha redio cha Jeshi la Israeli kilisema siku ya Jumatatu.

Siku ya Jumanne, Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki ililaani Israel kwa kukiuka Makubaliano ya mwaka 1974 ya kujitenga na kuingia katika ardhi ya Syria.

Magaidi wa PKK/YPG walenga kutumia mwanya wa kiusalama

Kundi la kigaidi la PKK/YPG linajaribu kutumia mwanya wa kiusalama kufuatia kuanguka kwa utawala wa Assad.

Katika kampeni yake ya miaka 40 dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK kiliorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, huku ikuhusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake, watoto wachanga na wazee.

Kikundi cha YPG ni kichipukizi cha kikundi cha PKK kwa upande wa Syria, eneo ambalo kikundi hicho kimekita kambi kwa muda mrefu na kutengeneza shoroba ya kigaidi katika mpaka wa Uturuki.

Katika miaka ya hivi karibuni, Uturuki imetuma wanajeshi na kufanya kazi na washirika wa ndani kama vile Jeshi la Kitaifa la Upinzani la Syria ili kuzuia hili na kuwaweka wenyeji salama kutokana na ukandamizaji wa kigaidi.

Kauli ya Erdogan yanakuja huku kukiwa na mwelekeo wa kimataifa kuhusu mustakabali wa Syria, huku wahusika mbalimbali wakijaribu kuchagiza mwelekeo wa nchi hiyo baada ya vita.

Mara kwa mara, msimamo wa Uturuki umesisitizia ushirikiano na watu wa Syria na kuzuia mgawanyiko wowote au unyonyaji wa ardhi ya nchi hiyo.

TRT Afrika